Meneja
wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (wa pili kulia) akiongoza vijana
wake kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani
ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mwimbaji
Baby, Ashura Kitenge pamoja na Sam Mapenzi.
Ijumaa
hii Skylight Band hawatopiga Thai Village watakua njiani wakitokea
nchini Oman, wanaomba radhi kwa usumubufu wowote utakaojitokeza kwa
wateja wao.
Ila
siku ya Jumamosi siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Skylight Band
wataporomosha burudani ya nguvu na ya aina yake kwa mashabiki wao ndani
ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku mashabiki wakipata
fursa ya kuchagua nyimbo wazipendazo zinazoendana na siku hiyo maalum
pamoja na kugawa zawadi kwa “couples” itakayonoga na kutokelezea.
I’m
Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)…I’m
Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,…..(Aiyayaaaaa)…Mmm Take
Me,….Nitembee Nawe,…..Baby Take Me, Nitembee Nawe….Aneth Kushaba AK47 akipiga kolabo na Sam Mapenzi.
Kikosi kazi cha Skylight Band wakisakata lisebene.
Moja
ya zawadi ndani ya usiku maalum wa Valentine’s ni hii Membership card
aliyoshika mdau Francis Machibya, ambayo inakupa nafasi ya kuhudhuria
show zote za Skylight Band zinazofanyika Thai Village bure kwa mwaka
mzima.
Comments