Wakati
Bobbi Kristina akiwa bado Hospitalini, Mwanasheria wa Baba yake amesema
kwa sasa wanafanya uchunguzi kubaini kilichomsababishia Bobbi Kristina
kulazwa.
Mwanasheria Christopher Brown amesema Mtoto wa waimbaji
Marehemu Whitney Houston na Bobby Brown hakuwahi kuolewa na Nick Gordon
kama ambavyo ripoti kadhaa zimekuwa zikidai.
Bobbi Kristina Brown
alikutwa akiwa amepoteza fahamu akiwa bafuni mwishoni mwa juma. Familia
yake imekuwa kimya kuhusu hali yake, lakini Baba yake alitoa taarifa
kupitia mwanasheria wake siku ya jumanne.
Bobby Brown ameomba jamii iache ishughulikie mambo ya kifamilia kwa uhuru na kumuonesha upendo bintiye.
Binti
huyo alifikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa hakuwa na fahamu
hali iliyowafanya kumkimbiza hospitali, mpaka siku ya jumatatu jioni
alikuwa bado kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Siku ya jumanne
alihamishiwa kwenye Hospitali ya Chuo cha Emory mjini Atlanta, Vyanzo
vilivyo karibu na Familia ya Brown vimeeleza.BBC
Comments