Raia wa
Nigeria wanatakiwa kushiriki uchaguzi wa urais Februari 14 ili kumchagua
au la Goodluck Jonathan kwa muhula wa pili kwenye kiti cha urais,
wakati ambapo rais huyo amekua akikosolea kwa kushindwa kukomesha
mashambulizi ya Boko Haram tangu alipoingilia madarakani.
Wakati
uchaguzi huo ukikaribia, Boko Harama imezidisha mashambulizi katika
baadhi ya maeneo ya Nigeria, na kudhibiti baadhi ya maeneo ya kaskazini
mwa nchi. Wakati Hata hivyo kulitokea mlipuko Jumatatu wiki hii katika
mji wa Gombe ambapo Goodluck Jonathan alikua akiendesha mkutano na
wafuasi wake, mara baada ya mkutano huo kumalizika.
Mlipuko
huo ulitokea katika kituo cha magari mbele ya uwanja wa mpira, ambapo
muda mchache kabla kulikua kukifanyika mkutano kati ya Goodluck Jonathan
na wafuasi wake, katika mji wa Gombe, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Mlipuko
huo umetokea mara tu baada ya msafara wa rais kuondoka eneo hilo. Watu
wawili wamefariki katika shambulio hilo na wengine zaidi ya ishirini
wamejeruhiwa. Wanawake wawili wanashukiwa kutekeleza shambulio hilo.
Kwa
mujibu wa mashahidi, makumi ya ya vijana waliandamana baadae katika mji
wa Gombe dhidi ya Goodluck Jonathan, kwa sababu, kama walivyobaini
mashahidi hao, chanzo cha shambulio hilo ni ziara ya rais.
Ni kwa
mara ya kwanza kundi la Boko Haram linaendesha shambulio likimlenga rais
Goodluck Jonathan. Hii ni hali ya hatari ambayo inamkabili rais
Goodluck Jonathan, siku chache kabla ya uchaguzi wa urais.
Boko
Haram iliendesha hivi karibuni mashambulizi mengine mwishoni mwa juma
lililopita dhidi ya mji mkuu wa Maiduguri. Hata hivyo Jumapili juma
lililopita, Boko Haram iliendesha mashambulizi katika mji mkuu wa jimbo
la Borno. Lakini jeshi na vikosi vya kiraia vya ulinzi walifaulu
kuwarejesha nyuma wanamgambo wa Boko Haram, baada masaa matatu ya
mapigano.
Hayo
yakijiri, Chad iliwatuma hivi karibuni majeshi yake nchi Nigeria na
Cameroon ili kukabiliana na mashambulizi ya Boko Haram, ambayo
yamekithiri.
CHANZO:R.F.I
Comments