Mashabiki wangeweza kupoteza maisha katika ghasia zilizoathiri nusu
fainali ya Kombe la Afrika, rais wa chama cha FA-Ghana aliiambia BBC.
“Tuna bahati hatujapoteza maisha ya mtu yeyote, japo kuna
waliojeruhiwa kutokana na vitu vilivyorushwa kwao,” alisema mkuu wa
FA-Ghana Kwesi Nyantakyi.
Mchezo ulisimamishwa kwa dakika 30 wakati mashabiki wenyeji
walipogomea mechi ambapo Ghana waliwafungwa wenyeji Equatorial Guinea
3-0.
Polisi walitumia mabomu ya machozi wakati makopo na mawe yaliporushwa na mashabiki wa nyumbani.
Kundi kubwa la mashabiki wa Ghana walikuwa salama nyuma ya lango,
wakati mashabiki pinzani waliporusha mawe ndipo helikopta ilipoamua
kusimamia ulinzi katika dimba la Malabo.
Comments