Nusu fainali ya Kombe la Afrika kati ya Ghana na wenyeji Equatorial
Guinea ilikuwa kama “kanda ya vita, “baada ya mechi kusimamishwa kwa
zaidi ya dakika 30 baada ya ghasia za watu.
Wachezaji walirushiwa makopo, mashabiki wa Ghana walikuwa salama
nyuma ya goli, polisi walitumia mabomu ya machozi na helikopta kuulinda
uwanja.
“Ni kama uwanja wa vita,” Chama cha soka cha Ghana kilituma ujumbe
kwenye twitter kikidai kuwa ni “vitendo vya kijinga vya kiharibifu” na
“ghasia za mashambulizi” zinatokea uwanjani.
Mechi ilipoendelea Ghana ilishinda 3-0 na kufudhu fainali ya
Jumapili, ambapo watacheza na Ivory Coast, ambao waliifunga DR Congo 3-1
siku ya Jumatano.
Fujo zilianza wakati wa mapumziko kati ya Ghana na Equatorial Guinea.
Comments