Kati
ya wapiganaji 20 au 25 wa kikundi cha IS hapo jana walijaribu kuingia
kwenye kambi ya mafunzo ya vikosi 400 vya Iraq na marekani huku wakiwa
wamevaa sare za jeshi la Iraq.
Wapiganaji hao waliuawa kwa shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa
Iraq na hakuna ofisa yeyote wa Marekani ambaye aliathirika na shambulizi
hilo.
Taarifa iliyotolewa na muungano huo imethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo.
Taarifa iliyotolewa ilikuwa inasema hivi ” kundi dogo la wapiganaji
wa ISIS waliokuwa wamevalia sare za jeshi la Iraq walivamia ngome yetu
ya Al Asad Air Base jimboni Anbar muda wa saa 7:20 asubuhi”.
Comments