Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuandaliwa kuwa somo la digrii ya miaka minne katika chuo kikuu nchini Canada.
Chuo Kikuu cha British Columbia Okanagan kinatarajia kutoa digrii ya
Sayansi ya Jamii (Sociology) ikilenga umuhimu wa umaarufu wa Cristiano
na athari yake kwenye jamii.
Japokuwa kozi hiyo haitegemea zaidi nguvu za kupiga mipira iliyokufa
(free kicks), Profesa Lus Aguiar amesema nyota wa Real Madrid
atazungumziwa zaidi.
Katika mahojiano ya hivi karibuni alisema; “Ronaldo ndio mjadala
mkuu, makutano ya darasani yatamhusu Ronaldo. Kisha tutachunguza, na
kupanua maudhui zaidi.
“Tutaanza na Ronaldo lakini Ronaldo ni kama mwanzo wa kuanza kujadili
masuala makubwa ambayo yana umuhimu katika jamii zaidi ya biografia ya
Ronaldo.”
Moja ya masomo (module) katika digrii hiyo inaitwa “The commodification of Cristiano Ronaldo”.
“Lakini sijui kama Ronaldo anajua chochote kuhusu kozi.”
Chuo Kikuu cha Staffordshire kinatoa kozi kama hiyo ya David Beckham.
Comments