Majaribio makubwa ya chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola yamepangwa kufanyika nchini Liberia.
Matarajio
ni kwamba zaidi ya watu elfu thelathini watajitokeza katika zoezi hilo
kubwa la majaribio ya chanjo hiyo iliyotengezwa na kampuni mbili za GSK
na Merck.
Katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita zaidi ya watu elfu tisa wamefariki
katika mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo ambapo Mataifa ya Afrika Magharibi
yaliathirika sana na ugonjwa huu.
Comments