Muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha anatarajia kutoa video
ya albamu yake mpya iitwayo ‘Haribu Mipango ya Shetani’ mwishoni mwa
mwezi ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mbasha, alisema maandalizi ya video
hiyo, yanaendelea vyema ingawa, hakuweka wazi ni kampuni gani itatumika
kuifanya kazi hiyo.
Aidha, Mbasha amewashukuru mashabiki wake kwa kuipokea albamu hiyo.
Amewataka wakae tayari kwa ajili ya video hiyo, ambayo anaamini mashabiki wataipenda.
“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuniunga mkono, nawaomba waendelee kuniombea niweze kukamilisha video hiyo,” alisema.
Comments