Mwandishi wa Al-Jazeera Peter Greste amesema hatapumzika mpaka
wenzake wawili waachiwe kutoka gerezani nchini Misri, imesema familia
yake.
Baada ya kukaa grezani kwa siku 400, Greste aliachiwa huru na
kusafirishwa siku ya Jumapili. Alitua salama nchini Cyprus, akielekea
kwao Australia.
Alikamatwa mwaka 2013 na kusomewa mashtaka dhidi ya kusambaza taarifa za uongo na kukisaidia chama cha Muslim Brotherhood.
Wenzake wawili wa Al-Jazeera, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed, bado wako jela.
Fahmy, ambaye ana uraia wa Misri na Canada, anaweza kuachiwa baada ya kukana uraia wake wa Misri, chanzo cha rais kimeeleza.
Ila hali bado iko kwa Mohamed, ambaye hana uraia wa nchi mbili.
Greste alizungumzia suala la wafanyakazi wenzie kwa familia yake baada ya kuachiwa.
Comments