Kocha Mkuu wa Ghana, Avram Grant amefurahia timu yake kutinga hatua ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika.
Grant amesema "Kufikia fainali si jambo rahisi kwa kuwa kuna timu nyingi bora na kubwa zimeishia njiani.
Ghana imetinga fainali baada ya kuwagalagaza vibaya wenyeji Guinea ya Ikweta kwa mabao 3-0 katika mechi ya nusu fainali.
Kocha huyo amesema kikosi chake chenye wachezaji wengi vijana kimeonyesha kina hamu ya kufikia mafanikio.BBC
Comments