Walimu wapatao 700 nchini Kenya wamekataa kurejea kufanya kazi
kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo wakiwahofia wanamgambo wa Kiiislamu wa
Somalia.
Mwaka uliopita, al-Shabab walilishambulia basi karibu na mpaka wa
Somalia, na kuua zaidi ya walimu 20 waliokuwa wakisafiri kwa ajili ya
Christmas.
Walimu hao waliogoma wameomba kuhamishiwa sehemu salama zaidi.
Wizara ya elimu ilisema itafikiria kuchukua hatua za kinidhamu tendo hilo endapo walimu hao hawatarudi kazini.
Mamia ya walimu wamekuwa wakifanya mgomo nje ya wizara ya elimu katika mji mkuu, Nairobi, wakitaka kuhamishwa shule nyingine.
Kaunti zilizoathiriwa na mgomo huo ni Garissa, Mandera na Wajir,
ambapo wanamgambo wa al-Shabab waliua zaidi ya watu 100 mwaka uliopita.Chanzo ni http://taarifa.co.tz
Comments