Mapigano
yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine, husuasn pembezoni mwa mji
wa Debaltsevo, ambapo waasi wanaooungwa mkono na Urusi wanajaribu
kuuzingira huo au kuushambulia.
Watu wengi wameuawa na makumi waliojeruhiwa, wamesafirishwa katika hospitali mbalimbali mji huo
Kwa
mujibu wa mwanahabari wa RFI nchini Ukraine, Sébastien Gobert, takribani
wanajeshi 200 wamejeruhiwa na wengi wao wako katika hali ya maututi.
Wapiganaji
wanaoungwa mkono na Urusi mashariki mwa Ukraine wamebaini kwamba wako
tayari kuwahamasisha vijana laki moja kujiunga nao wakati huu Marekani
pamoja na mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi Nato,
wakitarajia kutoa silaha kwa wanajeshi wa serikali ya Ukraine.
Hayo
yanajiri wakati mapigano makali yemeendelea kati ya vikosi vya serikali
na waasi hao wanapigania udhibiti wa eneo muhimu la usafiri la Debaltsev
mashariki mwa Ukraine.
Milio ya
risasi na milipuko ya mabomu ilisikika karibu na mji unaodhibitiwa na
serikali ya Ukraine wa Debaltsevo, mji ulio muhimu na ulio karibu na
miji miwili ya Donetsk na Luhansk, inayodhibitiwa na waasi wanaoiunga
mkono Urusi.
CHANZO:R.F.I
Comments