Maelfu ya riaa wa Jordan wameandamana katika mji mkuu , Amman, wakiunga
mkono serikali yao katika vita inavyotekeleza dhidi ya kundi la Islamic
State baada ya kumuua rubani wa ndege za vita wa Jordan.
Serikali
ya Jordan inasema kuwa ndege zake za vita zilifanya mashambulizi kadhaa
ya angani zikilenga wapiganaji wa Islamic State huko Syria Alhamisi.
Maafisa
wa usalama wa Jordan wanaarifiwa kuwa ndio waliokuwa wakilengwa na
mashambulizi huko Raqqa, eneo lenya ufuasi mkubwa wa IS nchini Syria.Source BBC.
Comments