Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2015

Mbasha Kuachia Video Mpya Mwezi Ujao

“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuniunga mkono, nawaomba waendelee kuniombea niweze kukamilisha video hiyo,” alisema Flora Mbasha Muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha anatarajia kutoa video ya albamu yake mpya iitwayo ‘Haribu Mipango ya Shetani’ mwishoni mwa mwezi  ujao. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mbasha, alisema maandalizi ya video hiyo, yanaendelea vyema ingawa, hakuweka wazi ni kampuni gani itatumika kuifanya kazi hiyo. Aidha, Mbasha amewashukuru mashabiki wake kwa kuipokea albamu hiyo. Amewataka wakae tayari kwa ajili ya video hiyo, ambayo anaamini mashabiki wataipenda. “Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuniunga mkono, nawaomba waendelee kuniombea niweze kukamilisha video hiyo,” alisema.

MWANA FA AKITETA JAMBO NA WAZIRI CHIKAWE NCHINI MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huyo alipokutana na Waziri huyo jijini Washington DC katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, na kwa upande wa Mwana FA yupo nchini Marekani kwa ajili ya matembezi yake binafsi hata hivyo alienda ubalozini hapo kwa ajili ya kumsalimia Balozi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na mwanamuziki mkongwe wa Bongo Flava, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA wakati mwanamuziki huy...

Chadema yavuta kasi mbio za urais Zanzibar

Dar/Zanzibar. Wakati NCCR-Mageuzi na CUF wakitangaza nia ya kugombea urais wa Zanzibar, Chadema bado wanaangalia mvumo wa upepo kabla ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuteua mwakilishi mmoja wa kupambana na CCM. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, ameshatangaza kujitosa kuwania nafasi hiyo, sambamba na Mwenyekiti wa NCCR wa Zanzibar, Ambari Khamis Haji. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema maandalizi ya ndani ya chama yanaendelea, huku pia vikao binafsi vya chama na kile cha Ukawa navyo vikifanyika kwa lengo la kupitisha jina la mgombea mmoja. CUF na NCCR Mageuzi Kujitokeza kwa Ambari, aliyegombea nafasi hiyo uchaguzi uliopita, kutaleta ushindani mkubwa ndani ya Ukawa na Maalim Seif. Ambari alisema uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo umetokana na uwezo wake na kukubalika na wananchi na sera za NCCR-Mage...

LAZARO NYALANDU ALIPOZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI, ARDHI NA MAZINGIRA YA NORWAY

Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu ( katika kati) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen (kushoto) wakiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Bi. Hanne-Marie Kaarstad, (kulia) Kabla ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam. Waziri waWizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway kwenye Mkutano uliofanyika Mpingo House jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira ya Norway, Mhe. Ola Elvestuen ( kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu baada ya Mkutano wa Kamati ya Bunge ya Maliasili, A...

WHO watoa ripoti mpya kuhusu Ebola

Shirika la Afya Duniani, WHO limetoa takwimu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Takwimu hizo zinazihusu nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia tu ambapo taarifa zinasema kumekuwa na wagonjwa 23 218 na vifo 9365. Mchanganuo wa takwimu hizo unaonyesha kuwa Sierra Leone imekuwa na wagonjwa 11 103, na vifo vya watu 3408, Liberia - wagonjwa 9007, vifo 3900 na Guinea - wagonjwa 3108 na vifo vya watu 2057. Takwimu hizo ni mpaka tarehe 15 Februari kwa nchi za Sierra Leone na Guinea, na Liberia ni mpaka tarehe 12 Februari. Pia Uingereza ilikuwa na mgonjwa mmoja bila kifo Takwimu kwa ajili ya Senegal, Nigeria, Hispania, Marekani na Mali zimeondolewa.Nchi hizo haziko katika karantini ya ugonjwa wa Ebola. CHANZO:BBC

Wabunge wazichapa mbele ya Rais Jacob Zuma

Bunge la Afrika Kusini lilikubwa na ghasia baada ya Wabunge wa mrengo wa kushoto kurushiana ngumi na usalama wakati hotuba ya mwaka ya Rais Jacob Zuma. Rais Jacob Zuma akitoa hotuba bungeni Chama cha Economic Freedom Fighters kinachoongozwa na Julius Malema, akirudia kumuingilia Zuma akitaka majibu ya skandali ya matumizi mabaya ya fedha. Julius Malema, kiongozi wa EFF naye pia alifukuzwa Spika wa bunge aliagiza kuondolewa, baada ya kuanzisha vurugu. Chama kikubwa cha upinzani, Democratic Alliance, walifanya mgomo baada ya kutolewa. Wabunge wa EFF wakishikana mashati na maafisa wa usalama “Huwezi kuleta polisi bungeni,” alisema kiongozi wa bunge Democratic Alliance Mmusi Maimane.

JK azindua Sera mpya ya Elimu, hoja za Mbatia zakumbukwa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Rais Jakaya Kikwete, amezindua sera mpya ya elimu ambayo pamoja na mambo mengine, imehusisha hoja za Mbunge wa kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, alizozitoa bungeni. Mbatia aliibua katika mikutano tofauti ya Bunge mwaka juzi na jana, akitaka serikali ipige marufuku matumizi ya vitabu tofauti vya mafunzo, kwa vile vinachangia kufifisha kiwango cha elimu nchini. Hoja za Mbatia aliyeingia bungeni na vitabu, akikosoa Sera ya Elimu na kuibua mijadala ndani na nje ya Bunge na kumpatia umaarufu zaidi hasa kisiasa. Jana, Rais Kikwete alizindua sera hiyo na kusema inalenga kuchochea uboreshaji wa elimu ikiwa ni pamoja kuruhusu matumizi ya kitabu cha aina moja kwa shule zote. “Sera hii inahimiza matumizi ya kitabu kimoja wakati wa kufundisha ili kuzisaidia shule zote nchini badala ya kutumia vitabu vya aina tofauti kama ilivyo sasa, hivyo kutakuwa na k...

Bei ya umeme kushuka Machi

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji nchini Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa habari Serikali imeshusha bei ya umeme nchini kwa asilimia 2.21 kuanzia mwezi Machi mwaka huu. Bei hiyo itatumika katika kipindi cha miezi mitatu wakati mapitio mapya yakiwa yanafanyika kulingana na mfumuko wa bei. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi, alisema hatua hiyo imekuja baada ya kupitia gharama ya uzalishaji wa umeme kwa kuzingatia mabadiliko ya bei ya mafuta, thamani ya shilingi ya Tanzania na mfumuko wa bei. Alisema  kufuatia bei hiyo mpya watumiaji wa majumbani  wamepunguziwa kwa shilingi nane kutoka Sh. 306 hadi Sh. 298. Watumiaji wa kati wanaotumia umeme wa Volti 400, bei itashuka kutoka Sh. 205 hadi Sh. 200 kwa uniti moja, sawa na punguzo la Shilingi tano kwa uniti. ...

IS wavamia ngome ya Marekani

  Kati ya wapiganaji 20 au 25 wa kikundi cha IS hapo jana walijaribu kuingia kwenye kambi ya mafunzo ya vikosi 400 vya Iraq na marekani huku wakiwa wamevaa sare za jeshi la Iraq. Wapiganaji hao waliuawa kwa shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa Iraq na hakuna ofisa yeyote wa Marekani ambaye aliathirika na shambulizi hilo. Taarifa iliyotolewa na muungano huo imethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo. Taarifa iliyotolewa ilikuwa inasema hivi ” kundi dogo la wapiganaji wa ISIS waliokuwa wamevalia sare za jeshi la Iraq walivamia ngome yetu ya Al Asad Air Base jimboni Anbar muda wa saa 7:20 asubuhi”.

Skylight Band kunogesha Valentine’s day ndani ya Thai Village Jumamosi hii..Usikose

Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 (wa pili kulia) akiongoza vijana wake kutoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kutoka kushoto ni mwimbaji Baby, Ashura Kitenge pamoja na Sam Mapenzi. Ijumaa hii Skylight Band hawatopiga Thai Village watakua njiani wakitokea nchini Oman, wanaomba radhi kwa usumubufu wowote utakaojitokeza kwa wateja wao. Ila siku ya Jumamosi siku ya wapendanao (Valentine’s Day) Skylight Band wataporomosha burudani ya nguvu na ya aina yake kwa mashabiki wao ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku mashabiki wakipata fursa ya kuchagua nyimbo wazipendazo zinazoendana na siku hiyo maalum pamoja na kugawa zawadi kwa “couples” itakayonoga na kutokelezea.  I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I, Love You, (Aiyayaaaaa)…I’m Going Koo Koo Koo, So Koo Koo Coz I, I Love You,…..(Aiyayaaaaa)…Mmm Take Me,….Nitembee Nawe,…..Baby Take Me, N...

TANZANIA YATANGAZA UTALII PARIS KUPITIA MAWAKALA WA UTALII

Baadhi ya wadau wa utalii wakimsikiliza Mh Balozi Begum Taj Wageni wakionja baadhi ya vyakula vya kitanzania. Ukarimu kwa wageni ni tunu ya watanzania. Picha ya jumla ya walioshiriki katika hafla ya kuitangaza Tanzania. Inatoka kwa Mjengwa

JK asema Diamond ni Msanii Bora

                             Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete Rais Jakaya Mrisho Kikwete siku chache zilizopita alimwagia sifa Msanii Diamond,wakati akihutubia wana CCM na wananchi kwa ujumla,katika sherehe za miaka 38 tangu kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi,Rais Kikwete alisema  Diamond ndio msanii bora barani Africa, hakuna zaidi yake kwa sasa..     

Bobbi Kristina bado yuko hospitalini

  Bobbi Kristina akiwa na Mama yake Marehemu Whitney Houston Wakati Bobbi Kristina akiwa bado Hospitalini, Mwanasheria wa Baba yake amesema kwa sasa wanafanya uchunguzi kubaini kilichomsababishia Bobbi Kristina kulazwa. Mwanasheria Christopher Brown amesema Mtoto wa waimbaji Marehemu Whitney Houston na Bobby Brown hakuwahi kuolewa na Nick Gordon kama ambavyo ripoti kadhaa zimekuwa zikidai. Bobbi Kristina Brown alikutwa akiwa amepoteza fahamu akiwa bafuni mwishoni mwa juma. Familia yake imekuwa kimya kuhusu hali yake, lakini Baba yake alitoa taarifa kupitia mwanasheria wake siku ya jumanne. Bobby Brown ameomba jamii iache ishughulikie mambo ya kifamilia kwa uhuru na kumuonesha upendo bintiye. Binti huyo alifikishwa hospitalini baada ya kugundulika kuwa hakuwa na fahamu hali iliyowafanya kumkimbiza hospitali, mpaka siku ya jumatatu jioni alikuwa bado kwenye chumba cha wagonjwa mahututi...

Mechi iligeuka Vichapo,Ghana yatinga fainali

Nusu fainali ya Kombe la Afrika kati ya Ghana na wenyeji Equatorial Guinea ilikuwa kama “kanda ya vita, “baada ya mechi kusimamishwa kwa zaidi ya dakika 30 baada ya ghasia za watu. Wachezaji wa Ghana wakishangilia ushindi wao dhidi ya wenyeji Equatorial Guinea. Ghana ilishinda 3-0 na hivyo kutinga fainali ambapo itapambana na Ivory Coast siku ya Jumapili Wachezaji walirushiwa makopo, mashabiki wa Ghana walikuwa salama nyuma ya goli, polisi walitumia mabomu ya machozi na helikopta kuulinda uwanja. Baadhi ya wachezaji wa Ghana wakilindwa na askari baada ya kurushiwa makopo na mashabiki wa E. Guinea. Mechi hiyo ilisimama kwa zaidi ya dakika 30 “Ni kama uwanja wa vita,” Chama cha soka cha Ghana kilituma ujumbe kwenye twitter kikidai kuwa ni “vitendo vya kijinga vya kiharibifu” na “ghasia za mashambulizi” zinatokea uwanjani. Helikopta ikisimamia ulinzi wa uwanja huo baada ya kuibuka ghasia. Mechi ilipoendelea Ghana ilishinda 3-0 na kufudhu fainali ya...

Somalia Yasitisha Uhamisho wa fedha

Hizi ni baadhi ya pesa zinazotumwa Somalia Benki zinazoshughulikia uamisho wa pesa kutoka katika familia za Wasomali wanaoishi Marekani kutumwa Afrika Mashariki zimefungwa kutokana na kitisho cha pesa hizo kusambazwa kwa wanamgambo wa Al Shabab. Wafanyabiashara wa benki kuu California hushughulikia hadi asilimia 80 ya uhamisho kutoka Marekani wenye thamani ya dola milioni 200 kwa mwaka. Wakuu wa mabenki hayo wamesema hakuna uwezekano wa kuendelea na uamisho wa fedha kutokana na kugundulika kwa kanuni mpya chafu ya matumizi ya fedha hizo. Wajumbe kutoka Marekani wamesema ili litakuwa ni janga kwa Wasomalia wanaoishi Afrika Mashariki. Kuna wasiwasi kwamba baadhi ya fedha zinazotumwa zinaingia mikononi mwa wanamgambo wa Al shabab.

Cristiano Ronaldo kuanza kutumika katika Digrii Sayansi ya Jamii 'Sociology'

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kutolewa kama digrii ya Sayansi ya Jamii (Sociology) katika Chuo Kikuu cha British Columbia Okanagan cha nchini Canada Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuandaliwa kuwa somo la digrii ya miaka minne katika chuo kikuu nchini Canada. Chuo Kikuu cha British Columbia Okanagan kinatarajia kutoa digrii ya Sayansi ya Jamii (Sociology) ikilenga umuhimu wa umaarufu wa Cristiano na athari yake kwenye jamii. Japokuwa kozi hiyo haitegemea zaidi nguvu za kupiga mipira iliyokufa (free kicks), Profesa Lus Aguiar amesema nyota wa Real Madrid atazungumziwa zaidi. Katika mahojiano ya hivi karibuni alisema; “Ronaldo ndio mjadala mkuu, makutano ya darasani yatamhusu Ronaldo. Kisha tutachunguza, na kupanua maudhui zaidi. Adhabu ya Ronaldo imekwisha na anatarajiwa kurudi uwanjani dhidi ya mahasimu wao Atletico Madrid siku ya Jumamosi “Tutaanza na Ronaldo lakini Ronaldo ni kama mwanzo wa kuanza kujadili masuala makubwa ambayo yana u...

Angalia Sehemu ambayo Shambulizi Limetekelezwa huko Syria

Hii ni sehemu ambako shambulizi limetekelezwa Watu zaidi ya 70 wameuwa katika wilaya iliyo nje kidogo na mji wa Damascus kwenye shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la Syria baada ya waasi kushambulia ngome inayodhibitiwa na jeshi la hilo kwa kutumia  rocketi. Wachunguzi  wa haki za binadamu wanaofatilia vurugu zinazoendelea Syria wamesema kwamba katika shambulizi hilo watoto 12 na wapiganaji 11 ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha. Hivi karibuni vifo vya mashambulizi ya kutoka angani vimeongezeka nchini Syria.

HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KATIKA MTANANGE

Helikopta ikisimamia ulinzi wa uwanja huo baada ya kuibuka ghasia. Mashabiki wangeweza kupoteza maisha katika ghasia zilizoathiri nusu fainali ya Kombe la Afrika, rais wa chama cha FA-Ghana aliiambia BBC. “Tuna bahati hatujapoteza maisha ya mtu yeyote, japo kuna waliojeruhiwa kutokana na vitu vilivyorushwa kwao,” alisema mkuu wa FA-Ghana Kwesi Nyantakyi. Baadhi ya vitu vilivyorushwa uwanjani Mchezo ulisimamishwa kwa dakika 30 wakati mashabiki wenyeji walipogomea mechi ambapo Ghana waliwafungwa wenyeji Equatorial Guinea 3-0. Polisi walitumia mabomu ya machozi wakati makopo na mawe yaliporushwa na mashabiki wa nyumbani. Ukuta ukiwa umetapakaa damu Kundi kubwa la mashabiki wa Ghana walikuwa salama nyuma ya lango, wakati mashabiki pinzani waliporusha mawe ndipo helikopta ilipoamua kusimamia ulinzi katika dimba la Malabo.

Avram Grant :Kutinga fainali ni raha

      Ghana iliichapa Guinea ya Ikweta Mabao 3-0 Kocha Mkuu wa Ghana, Avram Grant amefurahia timu yake kutinga hatua ya fainali ya kombe la mataifa ya Afrika. Grant amesema "Kufikia fainali si jambo rahisi kwa kuwa kuna timu nyingi bora na kubwa zimeishia njiani. Ghana imetinga fainali baada ya kuwagalagaza vibaya wenyeji Guinea ya Ikweta kwa mabao 3-0 katika mechi ya nusu fainali. Kocha huyo amesema kikosi chake chenye wachezaji wengi vijana kimeonyesha kina hamu ya kufikia mafanikio.BBC

Raia wa Jordan waandamana kupinga IS

   Raia wa Jordan waandamana kupinga islamic state Maelfu ya riaa wa Jordan wameandamana katika mji mkuu , Amman, wakiunga mkono serikali yao katika vita inavyotekeleza dhidi ya kundi la Islamic State baada ya kumuua rubani wa ndege za vita wa Jordan. Serikali ya Jordan inasema kuwa ndege zake za vita zilifanya mashambulizi kadhaa ya angani zikilenga wapiganaji wa Islamic State huko Syria Alhamisi. Maafisa wa usalama wa Jordan wanaarifiwa kuwa ndio waliokuwa wakilengwa na mashambulizi huko Raqqa, eneo lenya ufuasi mkubwa wa IS nchini Syria.Source BBC.

Tazama hapa Inshu hii ya Jaguar

Hii ni ushahidi tosha kuwa beef kati ya  Jaguar na Iyanya haijaisha, ndio kwanza inaanza, Beef ilianza wakati Jaguar anafanya remix ya wimbo wake wa One Centimetre na Iyanya. Jaguar alisema Iyanya hana heshima kwa wasanii wa Kenya , Iyanya akajibu kuwa Jaguar ni msanii mvivu  na kwamba hayuko tayari kutangaza kazi yake Nchini Nigeria. Jaguar ajibu tuhuma za uvivu Hivi.  

BONDIA NYOTA KATIKA MASUMBIWI AKATALIWA KUINGIA AUSTRALIA

Mayweather akifungwa pingu kwenda jela kutumikia kifungo cha miezi mitatu mwaka 2012 Floyd Mayweather Jr, 37, hataruhusiwa kuingia Australia baada ya Idara ya Uhamiaji kukataa kumpa visa siku ya Jumatano. Mayweather akiwa na mwanasheria wake Karen Winckler pamoja na rapa 50 Cent Juni 2012 Anaweza kuitumia kushinda, kiukweli, hajawahi kupigwa ulingoni, hatahivyo, pambano lake kubwa limetokea nje ya mnara wa hempen, bondia huyo amekataliwa kuingia nchini humo kutokana na tabia mbovu za nyuma. Tangu atoke jela Mayweather ameendeleza rekodi yake ya kutokupigwa mapambano yote 47 Taarifa ilitolewa kwenye mtandao wa chang.org kumzuia kuingia nchini humo kwa sababu inaeleza kuwa, ‘alimfanyia vitendo vibaya mwenzie mbele ya watoto wake na kwenda jela baada ya kuwanyanyasa wanawake watano tofauti. Mayweather alianza kupigana mwaka 1996, na ameshinda mikanda mitano ya uzito tofauti Kufungiwa kwake kulithibitishwa na Waziri wa Uhamiaji Msaidizi, ...

Mrema apewa siku 80 kufanya uchaguzi TLP

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imetoa siku 80 kwa uongozi wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) kuhakikisha kinafanya uchaguzi wake wa ndani wa kuwapata viongozi wapya. Kauli hiyo imeitolewa baada ya baadhi ya wanachama wa chama hicho kufikisha malalamiko katika ofisi hiyo wakiiomba itangaze kwamba uongozi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrema umefikia kikomo. Mwenyekiti wa Kamati ya Ukweli na Maridhiano wa TLP Taifa, Joram Kinanda alimtuhumu Mrema kukiuka katiba ya chama hicho, kuongoza chama kidikteta, kuporomosha heshima ya chama na kujilimbikizia madaraka. Akizungumza ofisini kwake, Dar es Salaam jana, Msaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alisema baada ya kusikiliza pande zote zinazosigana ofisi hiyo iliwataka viongozi kuandaa uchaguzi. "Tuliwasikiliza wote upande wa Kinanda na upande wa Mrema ambaye alikuwa na sababu kwamba alishindwa kuitisha uchaguzi kutokana na hali yake ya afya lakin...