Huku zaidi ya asilimia 97 ya kura
zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Brazil, rais
Dilma Roussef ameshinda awamu ya kwanza ya kura hizo, lakini bado
hajapa ushindi unaohitajika ili kuzuia kuwepo duru ya pili.
Mpinzani wake wa karibu Aecio Neves amechukua nafasi ya pili.
Matokeo
haya hata hivyo yanamaanisha kuwa mgombea mwingine ambaye ni waziri wa
zamani wa mazingira Marina Silva ameondolewa kwenye kinyanganyiro hicho
hata baada ya kuonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa rais wa Brazil.
Takriban watu milioni 150 walipiga kura katika uchaguzi wa saba wa nchi hiyo tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1985.
Bi Rousseff aliendesha kampeni
yake akitumia rekodi yake ya kubuni programu ambazo zimesaidia kukwamua
mamilioni ya watu kutoka umaskini nchini Brazil.
Cha kushangaza zaidi katika uchaguzi huu ni dalili ya kupoteza uungwaji mkono kwa waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva.
Mwezi
mmoja uliopita Bi Silva alikuwa aking'aa kwenye kura ya maoni baada ya
kuchukua usukani kama mgombea wa urais kupitia kwa chama cha
Kisoshiolisiti kufuatia kuaga dunia kwa mgombea mwenza kwenye ajali ya
ndege.
Lakini mijadala yake isiyo ya kuridhisha na pia uamuzi wa
wapiga kura wa kutotaka kupigia kuya vyama vya zamani ina maana kuwa Bi
Silva amendoka kabisa kwenye kinyanganyiro hicho.Chanzo ni BBC swahili.
Comments