MWIMBAJI
mashuhuri duniani, Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter
Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake.
''Sijui
, lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu
duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown.
Saa
chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo
uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikae
kimya”.
Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet.
Hata
hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana
wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza
ikiwa hana cha kusema.
Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi.
Ugonjwa
huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja
aliyueingia nchini humo akiwa ameambukizwa Ebola alifariki wiki jana.
Chanzo: BBC
Comments