Patrick Phiri, kocha wa Simba, amesema atamwanzisha
mshambuliaji Amissi Tambwe na kipa ‘kinda’ Peter Manyika Jr katika mechi
yao ya raundi ya tano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi
ya Tanzania Prisons itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
mjini hapa Jumamosi.
Tambwe raia wa Burundi aliyeibuka mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, alikosa mechi ya watani wa jadi wiki iliyopita kwa kile ambacho kilielezwa na Phiri kuwa “ni dhaifu kukabiliana na mabeki wenye nguvu kama Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Mfungaji bora huyo wa Kombe la Kagame mwaka jana – Tambwe ataanza
katika mechi hiyo ambayo kocha huyo amesema hawana budi kushinda ili
kurejesha matumaini yaliyopotea ghafla kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.
“Niliamua kutomtumia Tambwe katika mechi yetu dhidi ya Yanga kwa
sababu mchezo wake ni wa polepole na asingeliweza kuwa tishio kwa mabeki
wa Yanga, Cannavaro na Yondani kwa sababu wanatumia nguvu nyingi,”
alisema Phiri na kuongeza:
“Ataanza katika mechi yetu inayofuata dhidi ya Prisons. Makipa Ivo Mapunda na (Hussein) Sharrif bado ni majeruhi, hivyo (Peter) Manyika atakuwa golini Jumamosi. Timu itaingia Mbeya kati ya Alhamisi na Ijumaa.”
Simba haijapata ushindi tangu kuanza kwa msimu huu wa VPL ikiambulia sare katika michezo yote minne ya mwanzo. Timu hiyo ya Msimbazi haijawahi kupata ushindi katika mechi za ligi hiyo tangu iifunge Ruvu Shooting 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam miezi saba iliyopita.
Tayari Kocha wa Tanzania Prisons, David Mwamaja ameshaweka wazi kwamba kikosi chake kilichopo kambini mjini hapa, hakitakubali kuwa timu ya kwanza kufungwa na Simba msimu huu na kimejipanga kuendeleza ubaya dhidi ya Wanamsimbazi Jumamosi.

CHANZO: NIPASHE.
Comments