Serikali
nchini Nigeria inasema inachunguza taarifa ya idadi kubwa ya wanawake
na wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram Kaskazini
Mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kwamba tangazo la kusitisha mapigano
lililotolewa na majeshi ya serikali.
Msemaji wa Serikali ya
Nigeria Mike Omeri, ameiambia BBC kuwa serikali ya Nigeria inajaribu
kuthibitisha kile kilichotokea. Mwanakijiji mmoja anasema wanawake na
wasichana arobaini wametekwa na kundi hilo.
Makubaliano ya
kusitisha mapigano yalitangazwa wiki iliyopita, lakini mashambulizi
yanaendelea na mpaka sasa haijajulikana kama wasichana wa Chibok zaidi
ya mia mbili waliotekwa na kundi la Boko Haram miezi sita iliyopita
wataachiwa huru kama serikali ya Nigeria ilivyosema.BBC
Comments