MWANAMUZIKI
tegemeo wa Malaika Band, Christian Bella ambaye kwa sasa ndiye mwimbaji
tishio zaidi wa muziki wa dansi hapa Bongo, ameenda Sweden kumsalimia
mkewe na mwanae.
Bella amekiambia chanzi kimoja kuwa atakuwa huko kwa muda usiopungua wiki mbili
kabla ya kurejea Tanzania na kuachia ngoma zake mpya kabisa.
Hii inaamanisha kuwa kwa mara nyingine tena Malaika Band italazimika kufanya maonyesho kadhaa mfululizo bila ya mwimbaji huyo kipenzi cha mashabiki wa bendi hiyo.
Mara
ya kwanza ilikuwa mwezi Disemba mwaka jana ambapo Bella aliiacha kwa
muda bendi hiyo na kwenda Sweden kujiunga na familia yake.
Miezi michache baadae akalazimika kwenda tena Sweden kuweka sawa nyaraka zake za kiuhamiaji.
Katika
maendeleo mengine, Christian Bella hivi majuzi alikuwa kwao Kinshasa
nchini Congo DRC ambapo pamoja na mambo mengine ya kifamilia, alinunua
mjengo wa maana ulioko jirani na Airport ya Kinshasa.
Comments