Daktari
wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea
amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya
mjini Newyork.
Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari
wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada
ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.
Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de
Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu
zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na
maambukizi hayo.
Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa
Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini
Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.BBC
Comments