Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake nane leo wamepata dhamana
katika Mahakama ya Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius, Martha Mtiko na Beatus Mmari.

Mdee na wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza
washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani
Kinondoni, walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf
iliyowataka watawanyike.
Shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya
mtaa wa ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika
kinyume na sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais.
Chanzo: Jamii Forums.
Comments