Lufingo
MSANII anayefanya tasnia ya filamu nchini Exaud Lufingo amesema kuwa
yukombioni kuingiza ujio wake mpya katika filamu iitwayo 'Nishida'
kupitia kampuni ya Pamoja Films.
Miaka miwiliiliyopita Lufingo alianza kuingiza sokoni ujio
wa filamu iliyoitwa Kisanduku , katika ujio huu msanii wa vichekesho
Senga pamoja na msanii mwingine wa kike maarufu kwa jina la Matumaini
ambao wote walishakuwa kivutio katika sanaa ya vichekesho Comeddy nchini
wamefanya poa katika ujio huo mpya.
"Ujio huu upo tayari kuuingia sokoni jumatatu ijayo kupitia kamapuni hiyo ya Pamoja
Films ya jijini Dar es Salaam ambayo tayari imekuwa ikisambaza filamu kadhaa
katika soko la filamu nchini,"alisema.
Lufingo alisema kuwa katika ujio huo amewashirikisha wasanii wa Commedy kutokana
na kuwa filamu yote ni Commedy na kuwalengo ni kulishika soko la filamu
kwa kutumia wasanii mbali mbali wakiwemo wa vichekesho.
Kwa mujibu wa meneja wa kampuni hiyo Ambwene Mwansasu alisema kuwa tayari
ujio huo umeisha kamilika na siku hiyo ya Jumatatu kunamatumaini makubwa ya
kuingia sokoni.
Katika ujio huo pia juna baadhi ya wasanii wengine katika tasnia hiyo
wataonekana licha ya hao waliotajwa.
Comments