MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi.
MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi,akihutubia umati wa wakazi wa manispaa ya iringa na katika mkutano wa hadhara wa chama hicho jana katika viwanja vya kihesa sokoni.(Picha na Friday Simbaya)
Wakazi wa kihesa akifuatilia mkutano juu ya lori.
Na Friday Simbaya
MAKAMU Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA), Taifa, Patrick Ole Sosopi, amemtaka vijana, wanawake na wazee wajitokeze kwenye daftar la ukazi ili kuwa wapigakura halali wakati uchaguzi za serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Desemba 14 mwaka huu pamoja hule uchaguzi mkuu wa 2015.
Alisema kuwa bila kufanya hivyo watakosa haki ya kuchagulia na kuchagua wakati chaguzi hizo.
Ole Sosopi ambaye kabla ya kuchaguliwa ngazi ya Taifa, alikuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Ismani mkoani Iringa na anat kuwasili jimboni kwake Jumatano.
Ole Sosopi katika msafara huo aliaambatana na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Iringa mjini Leonce Marto.
Hata hivyo Ole Sosopi aliwataka vijana kwa wazee wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali kupita chama hicho wakati uchaguzi wa serikali za mitaa utakafika hapo baadaye.Inatoka kwa Mjengwa.
Comments