Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na
zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa
mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma
ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo
akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili
jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani
Kilimanjaro.
Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani
siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa
Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa
4 asubuhi.
Magari maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani
kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia
uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya
kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.
Comments