Kilabu
ya taifa la Ugiriki Pas Lamia kimemtaka mchezaji wake kutoka Sierra
Leone John Kamara kutofanya mazoezi ama hata kuichezea kilabu hiyo kwa
mda wa wiki tatu kutokana na hofu za ugonjwa wa Ebola.
Kamara
alirudi nchini Ugiriki baada ya kuichezea timu ya taifa lake Sierra
leone katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya taifa bora barani Afrika
dhidi ya Cameroon.Kilabu hiyo ilimwambia mchezaji huyo kwamba uamuzi huo
unatoka katika wizara ya afya nchini humo.
''kilabu hiyo
imeniambia kwamba sifai kuwa na timu hiyo kwa muda wa siku 15 hadi 21
kwa kuwa nilienda barani Afrika kucheza na kwa sababu ya virusi vya
ugonjwa wa Ebola'',Kamara aliiambia BBC.
''Wameniambia wazi kwamba
ninafaa kukaa nyumbani ama naweza kusafiri kwenda ughaibuni kuiona
familia yangu lakini si kufanya mazoezi na kilabu hiyo''.
Sierra
Leone ililazimika kuandaa mechi yake dhidi ya Cameroon mjini Younde kwa
kuwa imepigwa marufuku kuchezea nyumbani na shirikisho la soka barani
Afrika kutokana na mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Hatua
hiyo ya kilabu ya Lamia inajiri licha kuwa hakuna kisa chochote cha
Ebola kilichoripotiwa nchini Cameroon na kwamba Mchezaji huyo hajasafri
kwenda Sierra Leone kwa takriban mwaka mmoja sasa.
Comments