Kocha wa timu ya Taifa ya Benin, Olle Didier Nicolle ametaja kikosi
cha wachezaji 18 kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa
Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mfaransa huyo ameita wachezaji 13 wanaocheza nje ya nchi hiyo akiwemo
kiungo Stephane Sessegnon wa West Bromwich Albion ya Uingereza kwa
ajili ya mechi hiyo ya Kalenda ya FIFA itakayoanza saa 11 jioni.
Wachezaji wengine katika kikosi hicho ni Didier Sossa (AS Dragons FC
de I’Oueme, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel,
Tunisia), Jodel Dossou (FC Liefering, Austria), Sessi D’almeida (FC
Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudo (JS Saoura, Algeria) na
Saturnin Allagbe (US Krake, Benin).
Steve Mounie (HSC Montpellier, Ufaransa), Farnolle Fabien (Clermont
Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (SM Caen, Ufaransa), Michael
Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux,
Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Benin), Nafiou Badarou (ASO
Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin), Fortune Ore
(US Krake, Benin) na Seibou Mama (US Krake, Benin).
Msafara wa timu hiyo utaanza kuingia nchini kesho (Oktoba 9 mwaka
huu) kwa nyakati tofauti, na utakuwa umekamilika (Oktoba 10 mwaka huu).
Timu hiyo itafikia hoteli ya JB Belmont.
Comments