Skip to main content

Hali yazidi kua tete kwa Miss Tanzania, BASATA Kumvua Taji La Miss Tanzania 2014, Wizara Waandaa Kikao

miss tanzania 2015
Sakata la lililojitokeza la mrembo wa Taifa wa mwaka huu ‘Redd’s Miss Tanzania 2014′, Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri, limeingia katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kueleza kuwa litamvua taji hilo endapo itabainika kweli alichakachua umri wake.

Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey Mwingereza, aliliambia NIPASHE jana kuwa baraza hilo linasubiri uchunguzi ukamilike na endapo watabaini kuna udanganyifu ulifanyika hawatakuwa na la kufanya zaidi ya kumvua taji.
Wakati Mwingereza akieleza hayo, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wanatarajia kukutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili sakata hilo la Sitti.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, alisema serikali imesikia taarifa za mkanganyiko kuhusiana na mrembo huyo hivyo imeamua kuitisha kikao ili kuanza kulifanyia kazi.
Nkamia alisema kamwe serikali haiwezi kukaa kimya pale ambapo jina la nchi linatajwa vibaya.
“Siwezi kukuambia hatua gani zitachukuliwa, ila kesho (leo) tutakuwa na kikao, serikali haiwezi kukaa kimya, kuna vyombo vyake vinalifanyia kazi,” alisema Naibu Waziri huyo.
Aliongeza kuwa yeye alikuwa nje ya Dar es Salaam, lakini tayari kuna maelekezo aliyoyatoa na yameanza kufanyiwa kazi na wizara hiyo.
Siku moja baada ya Sitti kutangazwa mshindi wa taji hilo, taarifa za mrembo huyo kuhusu umri wake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha kuwa ana miaka 25, hivyo hana sifa za kushiriki shindano hilo hapa nchini.
Nakala ya hati ya kusafiria ya mrembo huyo ambayo ilitolewa Februari 15, 2007 na muda wake wa kumaliza kutumika ukiwa ni Februari 14, 2017 yenye namba AB 202696 inaonesha Sitti ambaye pia anashikilia taji la Kitongoji cha Chang’ombe na Kanda ya Temeke, alizaliwa Mei 31, 1989.Pia taarifa nyingine zinazoone sha mrembo huyo ana miaka 25 ni zilizokuwa kwenye Taasisi ya Explore Talent, ikimtaja kwamba anaishi Dallas, Texas, urefu wake ni 5’8, umbo lake ni la kati, asili yake ni Mwafrika na rangi ya macho yake ni kahawia.
Juzi, Kamati ya Miss Tanzania iliyoko chini ya Mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, ilisema kuwa Sitti amezaliwa Mei 31, 1991 katika wilaya ya Temeke jijini kwa mujibu wa cheti chake cha kuzaliwa alichokionesha.
Lundenga alionesha cheti cha kuzaliwa cha Sitti ambacho kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Septemba 9, mwaka huu kikiwa na namba 1000580309 na kikimtaja baba yake ni Abbas Mtemvu Zuberi (Mbunge- Temeke) wakati mama ni Mariam Nassor Juma (Diwani- Temeke).
Hata hivyo, Lundenga alisema kuwa kamati yake inaendelea na uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo na endapo watabaini kuwepo na udanganyifu watamchukulia hatua mrembo huyo kwa kushirikiana na Basata.
Pia Lundenga na Sitti, walikanusha taarifa za mrembo kuwa kuwa na mtoto na kusema kwamba mwenye uthibitisho wa jambo hilo anatakiwa aliwasilishe kwa kamati ili hatua zichukuliwe.
Sitti aliibuka kidedea katika shindano la urembo la taifa lililofanyika usiku wa Jumamosi ya Oktoba 11 kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini na kuwashinda washiriki wenzake 29 waliokuwa wanawania taji hilo.
CHANZO: NIPASHE

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...