Kocha mkuu wa timu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri, amesema
kikosi chake kina ari ya juu ya ushindi na kitashuka uwanjani kuwakabili
wapinzani wao Prisons katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara
Jumamosi kwa tahadhari ili waweze kupata pointi tatu muhimu.
Simba iliondoka jijini Dar es Salaam jana asubuhi na jioni iliwasili salama Mbeya tayari kwa mchezo huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine.

Phiri aliliambia gazeti hili kwamba kila timu inapokuwa kwenye Uwanja
wa nyumbani hujiamini zaidi lakini wao wamejipanga kukabiliana na
ushindani kutoka kwa wenyeji wao Prisons.
Kocha huyo alisema ligi ya Bara msimu huu ni ngumu na ushindi unaweza kupatikana ugenini au nyumbani.
"Ligi ina ushindani na changamoto, lakini pia hakuna mwenye uhakika wa kushinda nyumbani, hata ugenini timu inaweza kushinda, hicho ndicho ninachokiamini mimi, soka limebadilika," alisema Phiri.
Aliongeza kuwa, kikosi chake kinatarajia kuanza mazoezi leo asubuhi na jioni wataendelea kujinoa ili kujiweka tayari kuwakabili wenyeji.
Naye Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema wameamua kwenda mapema Mbeya ili kutoa nafasi ya wachezaji kupumzika na hatimaye kuendelea na mazoezi kwa muda wa siku mbili.
Aveva alisema kuwa wanaamini mazoezi waliyofanya katika kambi ya Afrika Kusini itawasaidia
kuendelea kuonyesha kiwango cha juu na hatimaye 'kuzoa' pointi tatu za kwanza msimu huu."Timu imeshaenda Mbeya, tunaamini mambo yatakuwa mazuri huko ingawa hakuna timu ya kuidharau kwenye ligi hii," alisema Aveva.
Rais huyo aliongeza kuwa huenda timu hiyo ikacheza mechi ya 'ndondo' mkoani Iringa mara baada ya kumaliza mchezo huo Jumamosi.
Baada ya mechi ya Jumamosi, Simba itacheza mechi nyingine ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar itakayofanyika Novemba Mosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Wekundu wa Msimbazi wamecheza mechi nne na wana pointi nne mkononi wakati vinara wa ligi hiyo ni mabingwa watetezi, Azam ambao wana pointi 10 sawa na Mtibwa Sugar.
Kipa chipukizi, Peter Manyika 'Junior' anatarajiwa kusimama tena langoni katika mechi hiyo kutokana na makipa wengine, Ivo Mapunda na Hussein 'Casillas' kuwa majeruhi.

CHANZO: NIPASHE
Comments