Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2014

HAKUNA UBISHI SITTI MTEMVU KADANGANYA UMRI

Stori: Mwandishi Wetu LILE  sakata la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu kudaiwa kudanganya limeingia ukurasa mwingine kufuatia ufukunyuku wa gazeti hili kubaini kuwa, miaka 25 ndiyo sahihi kwake. Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu. Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya… Stori: Mwandishi Wetu LILE  sakata la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu kudaiwa kudanganya limeingia ukurasa mwingine kufuatia ufukunyuku wa gazeti hili kubaini kuwa, miaka 25 ndiyo sahihi kwake. Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu. Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya umri. MADAI YA JUKWAANI Awali, akiwa jukwaani kujitambulisha...

Mourinho amsifu Van Gaal

Mkufunzi wa timu ya Manchester Louis van Gaal amesisitiza kuwa hakuchukuwa jukumu kubwa la kumfanya Jose Mourinho kuwa miongoni mwa wakufunzi waliofaulu duniani. Mkufunzi huyo wa Chelsea aliyefanya kazi chini ya Van Gaal katika kilabu ya Barcelona amekuwa akimsifu Kocha Van Gaal kwa mafanikio yake pamoja na Bobby Robson. ''Amekuwa akizungumza kunihusu na namshukuru kwa hilo lakini amekuwa akijifanyia mwenyewe'' alisema Van Gaal. Wawili hao watakutana katika uwanja wa Old Trafford siku ya jumapili wakati ambapo Manchester United itakutana na Chelsea. Kwa mara ya kwanza walikutana miaka 17 iliopita wakati Van Gaal alipomkabidhi Mourinho kazi katika kamati ya kufunzi katika uwanja wa Barcelona.BBC.

Pamoja Films:Kuingiza Nishida Jumatatu hii

Lufingo MSANII anayefanya tasnia ya filamu nchini Exaud Lufingo amesema kuwa yukombioni kuingiza ujio wake mpya katika filamu iitwayo 'Nishida' kupitia kampuni ya Pamoja Films. Miaka miwiliiliyopita Lufingo alianza kuingiza sokoni ujio wa filamu iliyoitwa Kisanduku , katika ujio huu msanii wa vichekesho Senga pamoja na msanii mwingine wa kike maarufu kwa jina la Matumaini ambao wote walishakuwa kivutio katika sanaa ya vichekesho Comeddy nchini wamefanya poa katika ujio huo mpya. "Ujio huu upo tayari  kuuingia sokoni jumatatu ijayo kupitia kamapuni hiyo ya Pamoja Films ya jijini Dar es Salaam ambayo tayari imekuwa ikisambaza filamu kadhaa katika soko la filamu nchini,"alisema. Lufingo alisema kuwa katika ujio huo amewashirikisha wasanii wa Commedy kutokana na kuwa filamu yote ni Commedy na kuwalengo ni kulishika soko la filamu kwa kutumia wasanii mbali mbali wakiwemo wa vichekesho. Kwa mujibu wa meneja wa kampuni h...

Breaking News: Mwimbaji Chid Benz Akamatwa na Madawa ya Kulevya Airport

Kuna Taarifa kuwa Msanii Chid Benzi amekamatwa na Madawa ya kulevya Airport Dar es Salaam ambapo alikuwa anaelekea Mbeya Kufanya Show ya Instagram..Amekamatwa na Kete Kumi na nne za madawa ya kulevya , pia na Bangi Misokoto miwili ambazo zilikuwa katika mfuko wake wa Shati . Chid alikuwa ameongoza na Mwanamuziki Sheta ambae yeye aliruhusiwa kuendelea na safari Baada ya kuhojiwa inasemekana Chid Alijitetea kwa kusema ni kwa ajili ya matumizi yake Binafsi , Chid kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.Kwa sasa Inshu hii inaendelea kuripotiwa zaidi na mitandao ya habari kama www.thechoicetz.com

Hali yazidi kua tete kwa Miss Tanzania, BASATA Kumvua Taji La Miss Tanzania 2014, Wizara Waandaa Kikao

Sakata la lililojitokeza la mrembo wa Taifa wa mwaka huu ‘Redd’s Miss Tanzania 2014′, Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri, limeingia katika sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kueleza kuwa litamvua taji hilo endapo itabainika kweli alichakachua umri wake. Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey Mwingereza, aliliambia NIPASHE jana kuwa baraza hilo linasubiri uchunguzi ukamilike na endapo watabaini kuna udanganyifu ulifanyika hawatakuwa na la kufanya zaidi ya kumvua taji. Wakati Mwingereza akieleza hayo, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wanatarajia kukutana leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili sakata hilo la Sitti. Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, alisema serikali imesikia taarifa za mkanganyiko kuhusiana na mrembo huyo hivyo imeamua kuitisha kikao ili kuanza kulifanyia kazi. Nkamia alisema kamwe serikali haiwezi kukaa kimya pale ambapo...

Nigeria inachunguza utekaji mpya

Serikali nchini Nigeria inasema inachunguza taarifa ya idadi kubwa ya wanawake na wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kwamba tangazo la kusitisha mapigano lililotolewa na majeshi ya serikali. Msemaji wa Serikali ya Nigeria Mike Omeri, ameiambia BBC kuwa serikali ya Nigeria inajaribu kuthibitisha kile kilichotokea. Mwanakijiji mmoja anasema wanawake na wasichana arobaini wametekwa na kundi hilo. Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitangazwa wiki iliyopita, lakini mashambulizi yanaendelea na mpaka sasa haijajulikana kama wasichana wa Chibok zaidi ya mia mbili waliotekwa na kundi la Boko Haram miezi sita iliyopita wataachiwa huru kama serikali ya Nigeria ilivyosema.BBC

Mgonjwa wa Ebola agundulika Newyork

Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini Newyork. Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi. Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo. Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.BBC

MNYANGE NYANDA ZA JUU KUSIKI AFUNGUKA, APONDA USHINDI WA SITTI , ADAI ULIPANGWA MAPEMA

MARIA Itala, mama mzazi wa Maureen (kushoto) akiwa na binti yake. Na Michael Katona, Njombe MSICHANA Maureen Godfrey, ambaye ni mrembo wa Nyanda za Juu Kusini, akitokea Mkoa wa Njombe, amefunguka na kudai kuwa ni vigumu kwa warembo kutoka kanda hiyo kuweza kufika hatua ya fainali kwenye shindano la Mrembo wa Tanzania. Akizungumza baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye mashindano ya kumsaka Miss Tanzania, yaliyofanyika Oktoba 11, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, Maureen alisema wakati akiwa anashiriki shindano la 'Miss Nyanda za Juu' mkoani Iringa, aliambiwa na mmoja wa majaji, ambaye anatoka ndani ya Kamati ya Miss Tanzania, kwamba ni ndoto kwa warembo kutoka mikoa ya kusini kuweza kushinda taji hilo. “Hakuna warembo wazuri na wenye sifa kutoka kanda hiyo, hivyo si rahisi kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuweza kutoa mrembo atakayeweza kutwaa taji hilo,” alisema Maureen akimnukuu jaji huyo (jina tunalo). Mrembo huyo alisema kwa jinsi ambavyo ameona m...

Sasa Manyika Jr kuendelea kupewa nafasi langoni

Patrick Phiri, kocha wa Simba, amesema atamwanzisha mshambuliaji Amissi Tambwe na kipa ‘kinda’ Peter Manyika Jr katika mechi yao ya raundi ya tano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa Jumamosi. Tambwe raia wa Burundi aliyeibuka mfungaji bora wa VPL msimu uliopita, alikosa mechi ya watani wa jadi wiki iliyopita kwa kile ambacho kilielezwa na Phiri kuwa “ni dhaifu kukabiliana na mabeki wenye nguvu kama Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’. Mfungaji bora huyo wa Kombe la Kagame mwaka jana – Tambwe ataanza katika mechi hiyo ambayo kocha huyo amesema hawana budi kushinda ili kurejesha matumaini yaliyopotea ghafla kutwaa ubingwa wa ligi hiyo. “Niliamua kutomtumia Tambwe katika mechi yetu dhidi ya Yanga kwa sababu mchezo wake ni wa polepole na asingeliweza kuwa tishio kwa mabeki wa Yanga, Cannavaro na Yondani kwa sababu wanatumia nguvu nyingi,” alisema Phiri na k...

Simba matumaini kibao : yasaka ushindi sasa.

Kocha mkuu wa timu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri, amesema kikosi chake kina ari ya juu ya ushindi na kitashuka uwanjani kuwakabili wapinzani wao Prisons katika mechi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Jumamosi kwa tahadhari ili waweze kupata pointi tatu muhimu. Simba iliondoka jijini Dar es Salaam jana asubuhi na jioni iliwasili salama Mbeya tayari kwa mchezo huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine. Phiri aliliambia gazeti hili kwamba kila timu inapokuwa kwenye Uwanja wa nyumbani hujiamini zaidi lakini wao wamejipanga kukabiliana na ushindani kutoka kwa wenyeji wao Prisons. Kocha huyo alisema ligi ya Bara msimu huu ni ngumu na ushindi unaweza kupatikana ugenini au nyumbani. "Ligi ina ushindani na changamoto, lakini pia hakuna mwenye uhakika wa kushinda nyumbani, hata ugenini timu inaweza kushinda, hicho ndicho ninachokiamini mimi, soka limebadilika," alisema Phiri. Aliongeza kuwa, kikosi chake kinatarajia kuanza mazoezi leo asubuhi na jioni ...

Bingwa wa tenisi akerwa kuitwa ''kaka'.

Serena Williams Bingwa wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi aliyoyataja kuwa ya kibaguzi na kutojali ujinsia yaliotolewa na rais wa shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na dadaake Venus Williams. Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili'' . Hatahivyo afisa huyo alipigwa faini ya pauni 15,500 na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha. ''Nadhani matamshi hayo yamejaa ubaguzi na hayajali'' alisema Wiliiams. ''Sikuyapendelea hata kidogona nadhani watu wengi pia hawakuyapendelea''. matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalishtumiwa na shirikisho la mchezo wa Tenisi duniani...

Soma hii Story kutoka Ghafla!

Habari hii imeandikwa na website ya Ghafla ya Kenya kuhusu bifu la wasanii Diamond na Ali Kiba wameelezea mengi na wamelitoa kama somo kwa wasanii wa Kenya. Hiki ndo walichoandika : Kenya is so full of talent. From music to sports, Kenya is so blessed. This is why we have great musicians in Kenya. This is why our athletes are breaking and setting new worlds every time they travel out of the country to represent us. Our footballers too will someday albeit the likes of Wanyama and Oliech doing good abroad. But mine is a message, a simple message to our celebrities. Just like three stones need each other to support a pot, so you do. Let me give you a story. I am not good at story telling but on this, I normally become the best. Once upon a time, not long ago, there was a certain country. The country was so celebrated because of its heritage. It had great people; from leaders to footballers, the country reigned. Democratically, the country was regarded as the bes...

‘Nishakuwa na Hao Wenye Vyeo, Pesa, Majina But Sikuwa na Amani’

Diva Loveness wa Clouds Fm Kwa Mara Nyingine Amemuongelea Mpenzi Aliye nae Kwa Sasa Grazy GK Kupitia Blog yake, na Haya Ndio aliyoyasema: “ The secret life to My happiness is the love of My life.. i believe that Love is the Greatest Gift life can give you, nilipo separate na hao waliopita thought i’d never love again but you can’t rule your heart, My bae is sucha great Person and incredibly loyal , he is the only man who seduced me with not only his charm but also his intelligence , he is matured positive and optimistic , very Passionate . we always on dinner for two with flowers ,table settings and the conversation always Brilliant and lovely….. you know when we started dating i had a feeling that i wasn’t a good enough person for him and normally that feeling wuld have made me want to leave but this time i couldn’t because i was too much in love with him, and its not about the money or fame but amma grown up sitaki mtu anieleze nani an...

Serikali yafuta Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti

Serikali imefuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kuanzia mwaka huu ili kuboresha kiwango cha elimu nchini. Tamko hilo limetolewa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt.Shukuru Kawambwa wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tabora, kilichoko Manispaa ya Tabora. Alisema kuanzia mwaka huu, Serikali imeyafuta mafunzo hayo ikiwa ni mkakati maalumu wa kuboresha kiwango cha elimu ambapo walimu ambao wataajiri wakufundisha shule za msingi na sekondari, watatakiwa kuwa na elimu ya kiwango cha diploma na kuendelea. Aliongeza kuwa, kuanzia sasa Wizara yake inataka kusimamia ubora wa elimu na walimu ambao kuanzia mwaka huu, wale ambao wataajiriwa kufundisha katika shule za msingi na sekondari, lazima wawe na elimu ya kiwango cha diploma na wasiofikia kiwango hicho, watapewa fursa ya kujiendeleza bila tatizo. “Walimu wa shule za msingi na sekondari na wahitimu wa kidato cha sita waliopata daraja la 1-3 na kuchaguliwa kujiunga na ko...

Meya Tabora amiliki boda boda 400

Meya wa Manispaa ya Tabora, Gullam Hussein Dewji akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana, baada ya kutoka kwenye Baraza ka Maadili ya Viongozi, alikoitwa kuhojiwa kuhusu tuhuma za kujilimbikizia mali na matumizi mabaya ya madaraka. Picha na Rafael Lubava Meya wa Manispaa ya Tabora, Gulam Hussein Dewji ameshushiwa tuhuma nzito za kuidanganya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kushindwa kutangaza mali anazozimikiki zikiwamo pikipiki 422, licha ya kutakiwa kufanya hivyo kisheria. Sheria Namba 5 ya mwaka 2001 ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inamtaka kila kiongozi kujaza fomu za kutangaza mali zake na madeni na kuziwasilisha kwenye Sekretarieti hiyo kila mwisho wa mwaka. Meya huyo alisomewa mashtaka yake jana na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus mbele ya Mwenyekiti wa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Hamisi Msumi. Mwanasheria huyo ...

Ebola:Mchezaji wa S.Leone atimuliwa

John Kamara Kilabu ya taifa la Ugiriki Pas Lamia kimemtaka mchezaji wake kutoka Sierra Leone John Kamara kutofanya mazoezi ama hata kuichezea kilabu hiyo kwa mda wa wiki tatu kutokana na hofu za ugonjwa wa Ebola. Kamara alirudi nchini Ugiriki baada ya kuichezea timu ya taifa lake Sierra leone katika mechi ya kufuzu kwa michuano ya taifa bora barani Afrika dhidi ya Cameroon.Kilabu hiyo ilimwambia mchezaji huyo kwamba uamuzi huo unatoka katika wizara ya afya nchini humo. ''kilabu hiyo imeniambia kwamba sifai kuwa na timu hiyo kwa muda wa siku 15 hadi 21 kwa kuwa nilienda barani Afrika kucheza na kwa sababu ya virusi vya ugonjwa wa Ebola'',Kamara aliiambia BBC. ''Wameniambia wazi kwamba ninafaa kukaa nyumbani ama naweza kusafiri kwenda ughaibuni kuiona familia yangu lakini si kufanya mazoezi na kilabu hiyo''. Sierra Leone ililazimika kuandaa mechi yake dhidi ya Cameroon mjini Younde kwa kuwa i...

Stephen Keshi apata mrithi Nigeria

Shaibu Amodu ndiye kocha mpya wa Nigeria    Shirikisho La kandanda la Nigeria NFF limefichua kwamba Shaibu Amodu ndiye atakayechukua nafasi ya Stephen Keshi kama mkufunzi wa timu ya taifa ya Nigeria. Hatua hii imechukuliwa muda mfupi tu baada ya bw. Keshi kuiongoza Nigeria katika mechi waliyoshinda kwa mabao 3-0 ingawa hakuwa amepatiwa mkataba na kufufua matumaini ya Nigeria ya kufuzu kwa dimba la kombe la Afrika litakaloandaliwa huko Morocco mwaka ujao. Baada ya kufanya mkutano wa dharura, shirikisho la kandanda nchini Nigeria limeamua kumteua Amodu kuingoza timu ya taifa ya Nigeria katika mechi zake mbili zitakazochezwa hapo Novemba katika juhudi zao za kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Afrika. Hata hivyo wamesema mkufunzi wa kudumu kutoka nchi za kigeni ataajiriwa baadaye. Amodu anakabiliwa na wakati mgumu kwani lazima ashinde mech...

MWANAMUZIKI KIONGOZI MALAIKA BAND KUTIMKIA SWIDEN

MWANAMUZIKI tegemeo wa Malaika Band, Christian Bella ambaye kwa sasa ndiye mwimbaji tishio zaidi wa muziki wa dansi hapa Bongo, ameenda Sweden kumsalimia mkewe na mwanae. Bella amekiambia chanzi kimoja  kuwa atakuwa huko kwa muda usiopungua wiki mbili kabla ya kurejea Tanzania na kuachia ngoma zake mpya kabisa. Hii inaamanisha kuwa kwa mara nyingine tena   Malaika Band italazimika kufanya maonyesho kadhaa mfululizo bila ya mwimbaji huyo kipenzi cha mashabiki wa bendi hiyo. Mara ya kwanza ilikuwa mwezi Disemba mwaka jana ambapo Bella aliiacha kwa muda bendi hiyo na kwenda Sweden kujiunga na familia yake. Miezi michache baadae akalazimika kwenda tena Sweden kuweka sawa nyaraka zake za kiuhamiaji. Katika maendeleo mengine, Christian Bella hivi majuzi alikuwa kwao Kinshasa nchini Congo DRC ambapo pamoja na mambo mengine ya kifamilia, alinunua mjengo wa maana ulioko jirani na ...

CHRIS BROWN ABWATUKIWA

  MWIMBAJI mashuhuri duniani, Chris Brown ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu kuhusu ugonjwa wa Ebola na kutoa maoni yake. ''Sijui , lakini nadhani Janga la Ebola ni njia moja ya kudhibiti idadi ya watu duniani...janga hili linatisha kweli,'' aliandika Brown. Saa chache baadaye alionekana kufahamu uzito wa kauli yake na ambavyo uliwakera watu kwenye mtandao huo na baadaye kusema....''afadhali nikae kimya”. Ujumbe wa Brown ulisambazwa mara 16,000 kwenye mtandao wa Internet. Hata hivyo watu hawahukufurahia matamshi ya Chris Brown kwani walaionekana wakimjibu kwa ukali baadhi wakisema, mwimbaji huyo anapaswa kunyamaza ikiwa hana cha kusema. Janga la Ebola limesababisha vifo vya zaidi ya watu 4000 katika kanda fa Afrika Magharibi. Ugonjwa huo umeenea hadi Uhispania na nchini Marekani ambako mgonjwa mmoja aliyueingia nchini humo akiwa amea...

Jide sasa kuzindua MOG

Kuiona mechi ya Yanga, Simba 7,000/-

Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000. Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani Kilimanjaro. Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia sa...

Museveni agharamia Uganda Cranes

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amegharamia safari ya timu ya soka ya taifa Uganda Cranes kwenda Togo, kucheza mechi ya marudiano siku ya jumatano ya kufuzu kucheza fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kundi E. Msemaji wa Shirikisho la soka nchini Uganda Ahamed Hussen amefahamisha BBC kwamba Rais Museveni amewapatia dolla laki moja na efu arobuni kusafirisha timu ya Uganda Cranes kwenda Togo kwa mechi ya Jumatano. Hicho ni kikosi cha Uganda Cranes kilichovalia jezi nyekundu yaani yenye kuishia 42 na yenye 40 ni Togo. Katika mechi ya jumasi Uganda Cranes ilinyamazishwa na Togo kwa bao 1 kwqa nunge hivyo Uganda wanahitaji ushindi mechi ya Jumatano kuongeza matumaini ya nafasi ya kushiriki fainali ya kombe la Afrika mwaka 2015 nchini Morocco. Katika kundi hilo E Ghana ndiyo wanaongoza na alama 5 wakifatiwa na Uganda alama 4...

PICHA:NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA ZANZIBAR SALUM MWALIMU APOKELEWA KWA SHANGWE,KATIBU MKUU WA CHADEMA DK WILBROD SLAA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CHADEMA JOHN MNYIKA WAUDHURIA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akipokewa na viongozi wa chama hicho baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar akifuatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Wilbrod Slaa (kulia) na viongozi wengine wa chama hicho jana. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu (kulia) akikabidhiwa vifaa vya ofisi kutoka kwa mtangulizi wake,Bw. Hamad Yusuf (kushoto) wakati wa hafla ya kumkaribisha iliyofanyika kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini,Zanzibar jana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa.     Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) - Zanzibar,Bw. Salumu Mwalimu akiongea kwenye mkutano wa ndani baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama hicho Daraja bovu mjini Zanzibar jana.    Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeo...

PICHA:MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA MAFINGA

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi wa Mafinga wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa .  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana na Bi.Mwigavillo Ngole ambaye amesafiri mwendo mrefu kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM  Wazee wa Kimila wakiwa uwanjani kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo walimpa Uchifu na kumtambua kwa jina la  Galiendela Matuga .  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Johanes Kaguo akifungua mkutano na kuhutubia wananchi wa Mafinga ambapo alielezea kero mbali mbali zinazowakabili wananchi wa Mafinga kwa Katibu Mkuu wa CCM.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafinga na kuwaambia kuwa Mafinga hamna upinzani ila kuna manung'ung'uniko ya wananchi ambao hawapati taarifa za kina kuhusu masula yanayohusu ugawaji na upatikanaji wa vibali vya mbao.  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca...