Dar es Salaam. Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba
na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa
huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.
Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa
mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa
hayo.
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii
Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa
Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya
zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.
Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa
nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika
Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za
kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni
(Sh125 bilioni).
Kaniki na Matumla walikamatwa Agosti 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Ndege wa Bole, Addis Ababa wakati wakijiandaa kupanda ndege ya Shirika
la Ndege la Ethiopia tayari kwa safari ya kuelekea Paris, Ufaransa.
Comments