Manchester City imeifunga Hull City
jumla ya magoli 2-0 katika uwanjani wake wa Etihad ,lakini licha ya
ushindi huo kiwango chake kilikuwa si cha kuridhisha sana.
Alikuwa ni Alvaro Negredo aliyetoka
benchi kuanza kuipatia Man City goli la kwanza huku Yaya Toure kufunga
bao la pili kwa mkwaju wa free-kick aliopiga kwa ustadi mkubwa.
Hull iliweza kupata nafasi kubwa za
kufunga bao katika kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji Sone Aluko
alishindwa kumalizia katika lango lililokuwa limeachwa wazi na kipa Joe
Hart.
Manchester City ilionekana bado
kutetereka katika safu yao ya ulinzi baada ya kukosa tena huduma za
mlinzi Vicent Kompany ambaye bado anauguza jeraha.
Comments