Na Anna Nkinda – Maelezo
Waumini ya dini ya Kiislam nchini wametakiwa kuwa pamoja katika
kuendeleza masuala ya kiimani bila ya kuhitilafiana kwani hititafu ndogo
huzaa migogoro katika jamii jambo ambalo linaweza kusababisha
kuvurugika kwa amani iliyopo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Wito huo umetolea jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa
ufunguzi wa msikiti na madrasa wa Masjid Madinatil Munawwar uliopo
Kibingu – Msanga Zalala kijiji cha Msimbu wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo (WAMA) alisema viongozi wa dini wanayo kazi kubwa ya
kuwasomesha na kuwaelimisha vijana wa Kiislam katika kumcha Mwenyezi
Mungu na kuwaasa juu ya kulinda amani iliyopo kwaajili ya maisha yao na
watu wengine.
“Naomba niwausie juu ya jambo hili kwani sisi wote ni waislamu ambao
tunaongozwa na kitabu kimoja na tunaabudu katika njia moja tusitumie
muda mwingi kuwa na marumbano kwenye misikiti yetu kuhusu imani.
Lakini pia tusiwe chanzo cha misuguano ambayo inaweza kuhatarisha amani
ya nchi bali tuwe na subira na kuvumiliana kama kuna tofauti yoyote
baina yenu mkae kwa pamoja na kutatua tatizo lililopo”, alitoa wosia
Mama Kikwete
Comments