Na Bosire Boniface, Garissa
Utulivu wa kiasi umerejea baina ya jamii za Gabra na Borana kwenye mpaka
wa Kenya na Ethiopia baada ya kuibuka kwa wasiwasi wa kisiasa uliovuma
wiki iliyopita, ukisababisha watu wapatao 12 kupoteza maisha na zaidi ya
60,000 kukosa makazi.
Mwonekano wa Moyale, mji ulio mpakani
ambao uko kando kando ya Kenya na Ethiopia, tarehe 22 Agosti, Vurugu
baina ya makabila ya Gabra na Borana katika wiki za hivi karibuni
ziliwaua watu wapatao 12 na zaidi ya 60,000 kukosa makazi. [Bosire
Boniface/Sabahi]
Kuibuka kwa vurugu wa hivi karibuni kulianza tarehe 22 Agosti wakati
watu watatu walipouawa huko Marsabit, na dereva wa lori kushambuliwa
kwenye njia kubwa ya magari itokayo Nairobi kwenda Moyale. Siku mbili
baadaye, watu wengine watatu waliuawa katika mapigano ya vita vidogo
baina ya jamii za Borana huko Moyale.
Kati ya tarehe 29 na 30, watu sita zaidi waliuawa na zaidi ya watu
20,000 walikimbia katika mpaka huo kuingia Ethiopia, ambayo iko umbali
wa chini ya kilometa moja kutoka mji wa Moyale, Mratibu wa Chama cha
Msalaba Mwekundu cha Kenya Stephen Bunaya aliiambia Sabahi.
"Takribani watu wengine 40,000 wanapiga kambi ndani ya shule nchini
Kenya," alisema. "Shule zimefungwa na wakati zitakapofungiuliwa familia
hizo zitapaswa kuondoka."
Umbali kutoka Moyale nchini Kenya na Ethiopia ni chini ya kilometa moja. [Bosire Boniface/Sabahi]
Wakati wa vurugu, Bunaya alisema nyumba zaidi ya 50 yakiwemo majengo ya biashara yalichomwa moto.
Comments