Waasi wa M23 wakiwa na silaha REUTERS/James Akena |
Na Victor Robert Wile
Umoja wa Mataifa, UN umewataka waasi wa kundi la M23 kuweka silaha chini
ili kumaliza mapambano yanayofanyika mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kuleta athari mbaya kwa wananchi.
Umoja huo umesema kumalizwa mapambano kati ya majeshi ya umoja huo na
waasi wa M23 kutasaidia kupatikana kwa njia za kuleta suluhu baina ya
pande hizo mbili.
Wito huo umetolewa na mjumbe maalum wa kanda ya Maziwa Makuu wa Umoja wa
Mataifa, Bi. Mary Robinson ametoa wito huo wakati wa ziara yake
mashariki mwa DRC eneo ambalo linakabiliwa na vita.
Hatua hiyo imekuja huku majeshi serikali ya Kongo yakishirikiana na
majeshi ya Umoja wa Mataifa yakiwa yamefanikiwa kuidhibiti ngome muhimu
ya waasi wa M23.
Bi Robinson akiwa mjini Goma baada ya kuzungumza na viongozi wa serikali
za mitaa na wakazi wa mji huo amesema kuwa waasi wa M23 lazima
wakomesheshe mapambano na kusalimisha silaha kama ilivyopendekezwa na
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Bi. Robinson aliwasli nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huku
majeshi ya DRC yakijipanga kuikomboa ngome ya Kibumba inayoshikiliwa na
waasi wa M23 iliyoko kilomita 30 kaskazini mwa Mji wa Goma.
Comments