Rais mpya wa Iran Hassan Rowhani amesisitiza kuwa nchi yake kamwe
haitakua na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia kama ambavyo imekuwa
ikidaiwa na Marekani na nchi za magharibi.
Rais mpya wa Iran Hassan Rowhani
Rais huyo amesema kuwa serikali yake itaelekeza nguvu kwenye mazungumzo
na nchi hizo na hivyo kukomesha hatua ya Iran kutengwa na dunia kwa
madai kuwa inalenga kutekeleza mpango wa nyuklia utakaozalisha silaha za
nyuklia.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC, tangu pale
alipo chaguliwa kuliongoza taifa la Iran mwanzoni mwa mwezi Agosti,
Rohani amethibitisha kuwa alikuwa na mawasiliano na rais Obama ambaye
alimuandikia risale.
Katika risala hiyo Rohani amesema Rais Obama alimpongeza baada ya
kuchaguliwa kuwa rais kuchukuwa nafasi ya Mahmoud Ahmednejad na kugusia
maswali mengine muhimu na ambapo alionyesha kuwa mtulivu.
Rohani ameendelea kusema, alijibu barua hiyo ya Obama na kumshkuru na
baadae kumpa maoni ya jamuhuri ya taifa la Iran, mtazamo wangu na risala
jiyo ilikuwa na ntazamo ulio chanya na wenye kujenga.
Comments