Wakenya wagawanyika kuhusu kura ya wabunge ya kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
Julius Kithuure alichangia katika ripoti hii kutoka Nairobi
Wakenya wametoa sauti ya kuwa na maoni tofauti kufuatia kura iliyopigwa
na watunga sheria Alhamisi (tarehe 5 Septemba) kurejesha mada ya
kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataiifa ya Makosa ya Jinai (ICC).
Msimamizi wa mgahawa jijini Nairobi
akiangalia matangazo ya habari za moja kwa moja tarehe 5 Septemba za
majadiliano kuhusu kujiondoa kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa
ya Jinai. [Simon Maina/AFP]
Kura hiyo ya ishara tu haitakuwa na athari kwenye majaribio yanayokuja
ya Makamu wa Rais William Ruto na Rais Uhuru Kenyatta, na bunge lazima
lipige kura baadaye kuhusu mswada huu ndani ya siku 30 kuweka hatua
rasmi kwa ajili ya kujitoa.
Mada ya majadiliano "kusimamisha muungano wowote, ushirikiano na msaada"
kwa mahakama kuliidhinidhwa kwa kishindo na Bunge la Taifa kupitia kura
ya maoni.
Hadi leo, nchi 122 ni sehemu ya Sheria ya Roma ambayo ilianzisha ICC, na
kama Kenya itajitoa ICC itakuwa ni mwanachama wa kwanza wa mahakama
hiyo kufanya hivyo.
Wakenya wakitembea nyuma ya jengo la bunge
jijini Nairobi tarehe 5 Septemba, tarehe ambayo wabunge walikuwa na
mjadala wa kujitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
[Simon Maina/AFP]
Wabunge wazungumza katika mjadala uliokuwa moto
Katika mjadala uliokuwa moto ambapo wabunge mara kwa mara waliomba
kuwepo kwa taratibu wakati walipokuwa wakichangia mada na wakishangiliwa
na wenzao, kiongozi wa wengi katika bunge Aden Duale alisema kujitoa
kutoka ICC kungelinda katiba ya nchi na kuhifadhi taswira ya Kenya".
Comments