Taasisi ya fursa ya Elimu (Opportunity
Education) ya nchini Marekani imeazimia kuanzisha mradi wa laptop ndogo
(tablets computer) kuanzia mwezi Januari mwaka 2014 nchini ambazo
zitatumika kufundishia ili walimu waweze kufundisha haraka na kwa
ufanisi zaidi pia wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza zaidi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments