Katika mkutano na waandishi wa habari
mjini Nairobi, waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa Kenya alitupilia
mbali swala kwamba serikali ya Kenya ingefaa kuzindukana baada ya kupata
habari mapema kwamba kuna uwezekano wa shambulio kubwa la kigaidi
kutokea katika mji mkuu.
Waziri Joseph Ole Lenku alilitoa
maanani swala hilo la mwandishi wa BBC na kusema kuwa taarifa za
ujasusi, yaani intelijensi, ni swala la serikali:
"Sifikiri kama weye ndie wa kuniambia mimi nini serikali ingefaa kusema au la.
Kuhusu taarifa na ujasusi wetu, hilo halijakuhusu.
Comments