KAMPUNI ya simu za
mkononi VODACOM Tanzania, imesema itaendelea kuchangia maendeleo ya elimu
nchini, kama sehemu yakurudisha , faida kutoka kwa wateja wake ,sanjari
nakushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo hususani elimu.
Hayo yalisemwa jana na
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa VODACOM Tanzania, Perece Kirigiti wakati wa
hafla fupi ya kuwaaga wahitimu wa kozi ijulikanayo kwa jina la “Discover
Program ,” iliyofanyika katika hoteli ya Seaclif Jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Akizungumza wakati wa
hafla hiyo Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa VODACOM Tanzania Perece, alisema kampuni
yao iliamua kuanzisha programu yakuwaendeleza wahitimu kutoka vyuo vikuu nchini
kwa lengo la kuwajengea uwezo kitaaluma katika eneo la uongozi.
Lengo la programu hiyo
nikuwapa uwezo wakuwa viongozi bora na mahiri katika masuala ya uongozi mahali
pakazi ili wawe na soko kubwa katika ulimwengu wa ajira na kuwawezesha
kuajiriwa katika makampuni na mashirika mbalimbali nchini.
“Tulianzisha programu hii
2015 tukizunguka katika vyuo mbalimbali nchini nakuchukuwa baadhi ya wanafunzi
ambao wamefanya vizuri katika masomo yao hususani wa shahada ya kwanza
natunawajengea uwezo katika kampuni yetu baadae huajiriwa ndani ya kampuni au
katika makampuni mengine,”Alisema
Perece alisema wahitimu
wanaopata nafasi ya kujifunza programu hiyo wanachukuliwa sawa na watumishi wa VODACOM na
wanapaswa kuishi kwakufuata sera,utaratibu na utamaduni wa VODACOM hakuna anaye
baguliwa kwa rangi,imani au kabila.
Gervas Mfumbusa alisema
alipokuwa akijifunza kwa vitendo katika kampuni hiyo alijitahidi kuwa mpole na
kujifunza jinsi wafanyakazi wenzake wanavyofanya kazi nakujifunza mazingira ya
kazi na baada ya miaka yake miwili amejikuta akipandishwa daraja nakuajiriwa
katika kitengo cha rasilimali watu VODACOM.
“Unapohitaji mafanikio
huna budi kuwa mtulivu ili uweze kufanikiwa katika kile unacho kihitaji ndivyo
nilivyofanya na nilikuwa nimejiwekea malengo ,kampuni inahitaji faida basi mimi
ntahakikisha mauzo ya kampuni yanaongezeka na kampuni inapata faida,”Alisema
Keisha Mushi mmoja wa
wahitimu hao alisema kuwa suala halikuwa kupata kazi au kufanya kazi kwa bidii,
suala la msingi kwake lilikuwa kujifunza kutoka kwa wakuu wa idara na
alijifunza mengi kutoka kwa viongozi wake na hatimaye alihitimu nakuwa mfanyazi
bora.
“Nimejifunza mengi
VODACOM kuliko nilivyo kuja hadi kufikia ngazi na mimi kuwa mkufunzi kwa
wengine,ushauri wangu ,ukitaka kufanikiwa kuwa mtiifu,jifunze kukubali kuwa
huwezi ili uweze,”Alisema
Jumla ya wahitimu kumi
wamehitimu katika kozi hiyo ya uongozi iliyozinduliwa 2015 ambapo wahitimu
walijifunza kwa takribani miaka miwili ambapo wameiva katika masuala ya uongozi
mahala pakazi.
Comments