Kampuni ya Bima ya Metropolitan imewapatia ufadhiri wanafunzi
wanaosoma shahada ya kwanza ya bima na udhibiti wa majanga katika Chuo cha
usimamizi wa fedha (IFM) kwakuwalipia ada wanafunzi watatu wa mwaka watatu
wanaosoma shahada ya kwanza ya bima na udhibiti wa majanga.
Makamu Mkuu wa Chuo cha IFM Dk. Emanuel Mzava aliwataja
wanafunzi hao kuwa ni Rhoda Carol, Leonard Mahimbo, na Paschalina Msofe wote
wakiwa mwaka watatu.
Akizungumza katika hafla ndogo ya kuwakabidhi wanafunzi hundi
ya shilingi milioni 4,500,000 iliyofanyika chuoni hapo Dk. Mzava alisema kuwa
Wakala wa Bima nchini (TIBA) wamekua wakiwatafuta wadau kwa ajili ya kuwasaidia
wanafunzi wanaosoma masomo ya bima na masomo mengine.
“Tunao mkataba wa kudumu na TIBA ambapo huwasaidia wanafunzi
wetu kuwaunganisha na makampuni ya bima kwakupatiwa mafunzo kwa vitendo, kupatiwa
kazi pamoja na ufadhiri wa kitaaluma,”amesema.
Dk Mzava aliongeza kuwa hata ufahiri uliotolewa jana na
kampuni ya Metropolitani ni matunda ya mahusiano mazuri na TIBA, IFM na Metropolitan
wana mkataba wa mda mrefu wakuwasaidia wanafunzi ambapo baadhi wamenufaika na
mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Metropolitan Suresh Kumar,
alisema tokea kuanzishwa kwa ushirikiano baina yao na IFM wanafunzi 11
wamenufaika na mpango huo na kuongeza kuwa baadhi ya wahitimu wa bima chuoni
hapo wameunganishwa na makampuni ya bima.
“Hatuishii kudhamini tu,vilevile tunaajili,na tunawaunganisha
na makampuni rafiki ya bima nchini lakini hatuwazuii kufanya kazi katika sekta
mbalimbali, wapo wanaofanya katika sekta za fedha yakiwemo mabenki,”amesema.
Kumar aliwasisitiza wanufaika wa ufadhiri huo kusoma kwa
bidii nakufanya vyema kwenye masomo yao hususani katika kipindi cha mwaka wa
mwisho kwakuwa soko la ajira hulenga zaidi waliofanya vizuri katika masomo.
Rhoda Caroli akizungumza kwa niaba ya wanafunzi walionufaika
na ufadhiri huo, aliuhakikisha uongozi wa IFM,TIBA na Metropolitani kuwa
watasoma kwa bidii na hawata waangusha kitaaluma.
“Kwa niaba ya wenzangu ,tunashukuru kwa ufadhiri huu
tunaahidi kuutendea haki na hatuta waangusha tutasoma kwa bidii ili kutimiza
malengo yetu ili tuweze kutoa mchango katika sekta ya bima na nchi yetu,”amesema
Comments