Rais wa Marekani
Donald Trump amezionya kampuni za mawasiliano ya mtandao Google, Twitter na
Facebook kwa kile alichokiita kuminya taarifa zake na za mrengo wa kihafidhina.
Trump ameitaka mitandao hiyo kuwa makini
baada ya awali kuishutumu Google kwa kupindua matokeo ya taarifa pale mtumiaji
wa mtandao huo anapotafuta habari kumhusu Trump.
Hata hivyo, Google wamekanusha shutuma kuwa
mtandao wao unaupendeleo na kusema hawafungamani na itikadi yoyote ya kisiasa.
Akiongea na wanahabari katika ikulu ya White
House, Trump amesema, "Google wamekuwa wakihadaa watu wengi, ni jambo zito
sana."
Akaziongeza pia kata lawama Twitter na
Facebook, "inawapasa wawe makini, hauwezi ukawafanyia watu mambo
haya…tunapokea maelfu ya malalamiko juu ya jambo hili."
Rais Trump hatahivyo hajabainisha ni hatua
gani hasa ambazo utawala wake unapanga kuzichukua.
Awali mshauri wa Trump wa masuala ya uchumi,
Larry Kudlow amesema utawala kwa sasa unaangalia ni namna gani wataliendea
suala hilo kwa kuangalia kanuni za udhibiti.
Comments