Sehemu ya waokoaji wakiwa katika pemezoni mwa kivuko cha Mv. Nyerere kilichopinduka na kupelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujerukiwa, katika eneo la Ukara, Kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza, wakiangalia maeneo mbalimbali kutafuta miili au watu waliohai waliozama kwenye maji. ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka juzi Alhamisi (Septemba 20, 2018) kikikadiriwa kubeba idadi kubwa ya abiria kuzidi uwezo wake. Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mpaka wahati huu miili ya waliopolewa majini imefikia 163, huku kati yao miili 116 imetambuliwa na ndugu zao. Picha zote na Kasampaida.
Vivuko vya Mv. Clarias na Mv. Nyehunge vikiwa tayari kwa msaada wowote wa hata.
Zoezi la Ukoaji likiendelea.
Baadhi ya vijana wa Skaut wakiwa wamebeba moja ya miili iliyoopolewa kwenye maji baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments