CHINA imefungua milango ya biashara ya mazao ya kilimo, ambapo Tanzania
imeombwa kupeleka bidhaa za kilimo zilizoongezwa thamani.
Pichani Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Biashara ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE)Edwin Rutagenika .
Katika hali hiyo zinahitajika tani 200,000 za mbaazi zilizokobolewa na zisizoko
bolewa natena wakati huo, zikihitajika tani 138,000 za tangawizi zilizoongezwa thamani.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Biashara ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE)Edwin Rutagenika
alipo rejea kutoka nchini China.
“Nilikuwa nchini China hivi karibuni,China imeridhishwa na bidhaa za kilimo
ambapo zinahitajika tani nyingi za mazao mbalimbali ya kilimo,”Alisema
Bidhaa za kilimo zilizooledheshwa ni pamoja na korosho,mbaazi,kahawa,
tangawizi, mhogo, choroko na kunde.
Rutagenika alisema kuwa wana jukumu la kukuhakikisha bidhaa na mazao yanayozalishwa
Tanzania yanapata soko ndani ya nchi na nje ya nchi, lakini alisistiza watanzania
kuzalisha bidhaa zenye ubora na zinazokidhi ushindani wa soko.
“Tuitumie hii fursa kwakuzalisha bidhaa zenye ubora na zilizoongezwa thamani na
zilizo fungashwa vizuri, wenzetu wa China wameonesha utayari wakununua bidhaa
zetu hatunabudi kuzalisha bidhaa zenye ubora ,”amesema Rutagenika.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo wa TANTRADE alisema kuwa atawafikishia ujumbe maofisa
kilimo,maofisa ushirika, maofisa biashara,wakurugenzi wa halmashauri,makatibu
tawala wa mikoa,wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhimiza uzalishaji
Uhuru liliongea na Ofisa kilimo kata ya Mpitimbi halmashauri ya Songea
vijijini David Chiza ili kujua amezipokeaje taarifa hizo,kwa upande wake
alisema kuwa ni taarifa njema na yupo tayari kuwahimiza wananchi kuweka mkazo
katika mazao yaliyotajwa hususani mbaazi.
“Kazi yetu nikutoa ushauri elekezi kwa wakulima na wanajitahidi lakini soko
limekuwa kizungumkuti, kuwe na mikataba baina ya wanunuzi na nchi washirika
ambao tutauzia nchi husika mana India ili tuangusha kwenye mbaazi lakini
masoko ya ndani ya imarishwe pia,”Amesema
Naye Subira mpwapwa mkulima wa korosho kutoka kijiji cha matemanga wilayani
Tunduru alisema taarifa hizo zinaleta matumaini lakini ameiomba serikali
kufuatilia kwa umakini kama walivyofanya katika msimu wa ununuzi wa korosho
mwaka jana.
“Wajanja wamekuwa wengi wana mbinu lukuki kila iitwapo leo,serikali isituache
peke yetu imetutafutia soko tutajitahidi kuzalisha kwa wingi lakini ombi langu
maofisa ugani wawe wanatutembelea marakwamara ili kuzibaini changamoto zetu
siyo hadi tuwafuate,”Amesema
Vilele TANTRADE imetoa wito wakuunganishwa kwa wafanyabiashara kuwa kitu kimoja ili
kulishinda soko hilo na wakati ukifika waende kama timu kuliko kila mtu kujiendea
kivyake na maofisa biashara kutoa ushauri wa kibiashara.
Comments