Nahodha wa kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' Mbwana Samatta, amesema hakuna haja ya wadau wa soka kuanza kuzungumzia wachezaji walioachwa na Kocha wa timu, Emmanuel Emmanuel na badala yake wanapaswa kuweka akili kuelekea mechi dhidi ya Uganda.
Samatta ambaye ndiye Nahodha Mkuu wa kikosi hicho, ameeleza kuwa kutolewa kwa wachezaji hao na Kocha Amunike haina maana ya kuwa si sehemu ya timu, bali wataendelea kuwa pamoja kwa kipindi chote.
Samatta ameamua kuzungumzia hilo kutokana na wachezaji 6 wa klabu ya Simba kutemwa na Kocha Amunike baada ya kuchelewa kuripoti kambini tofauti na muda uliokuwa umepangwa.
Licha ya kuchelewa, Amunike aliwasamehe wachezaji hao baada ya kukutana nao na akawaahidi kuwarejesha tena pale watakapomshawishi kwa kupambana kupitia klabu yao.
Comments