TANZANIA imezikaribisha nchi za Bara la Asia
na nchi za Afrika kuja kuwekeza nchini kutokana na rasilimali nyingi zilizopo
nchini.
Hayo yalisemwa jana na Balozi Hassan Yahya, wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mahusiano kati ya Afrika na Asia,
uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo wataalamu kutoka nchi za bara la Asia
na Afrika wemeshiriki.
Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
“Tunazo fursa nyingi za uwekezaji hapa nchini,tumieni fursa
za mkutano huu kubaini maeneo ya uwekezaji,nchi yetu ina mazingira mazuri ya uwekezaji
lakini utengamano na utulivu wakisiasa ni kichocheo cha uwekezaji nchini ,”Amesema
Balozi Yahya, aliuambia ujumbe wa wawashiriki wa mkutano huo
kutoka mataifa mbalimbali duniani kuwa miongoni mwa maeneo watakayo wekeza ni
katika, madini, elimu, afya, kilimo,utalii,biashara
na uchumi na sekta ya mawasiliano na uchukuzi.
Hata hivyo Balozi Yahya aliwataka washiriki hao kuwakaribisha
watanzania kuwekeza katika nchi za Asia kutokana na kuwa na rasilimali nyingi
ambazo nchi za Afrika zinaweza kuwekeza katika bara hilo.
“Naamini mkutano huu utatoa mwanga nakuanzisha ukurasa mpya
kwa Afrika dhidi ya Asia ambako kuna fursa nyingi za uwekezaji ili Afrika
iwekeze huko.,”Amesema
Kwaa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Profesa William Anangisye, alisema mkutano huo umekuja wakati muafaka ambapo
kuna majadala unaendelea kuhusu ajenda ya mahusiano ya kiuchumi kati ya Asia na
Afrika.
“Ninaamini kongamano hili litatoa wigo mpana katika ajenda ya
mahusiano ya uchumi baina ya mabara hayo mawili ili kuweza kushirikiana katika
fursa zinazopatikana katika mabara hayo,”Alisema
Profesa mstaafu wa magonjwa yasiyokuwa yakuambukizwa wa Chuo
Kikuu cha Tiba Muhimbili Zulfiqarali Premj, amesema mkutano huo ni muhimu na anaamini
Afrika na Asia zitanufaika na rasilimali zinazopatikana katika mabara hayo.
“Sisi tunataka matunda ya mahusiano yetu yawafikie wananchi
wa kawaida na siyo tabaka la juu tu,tupo hapa kujadili maslahi mapana ya uhusiano
wa kiuchumi kwa mataifa yaliyopo katika mabara hayo lakini ni jinsi gani
wananchi watanufaika.
Mkutano huo wa siku tatu umehudhuriwa na washiriki zaidi ya
mia nne kutoka nchi mbalimbali duniani na kuendeshwa na jopo la wataalamu
wasomi 100 wabobevu katika masuala ya uchumi na diplomasia.
Comments