CHAMA Cha waganyabiashara wenye Viwanda,Kilimo nchini (TCCIA)
kimesema kuwa ujio wa wawekezaji 20 kutoka nchini Taiwan wataweza kusababisha
nia ya wenye makamuni lengo la kufikia uchumi wa kati.
Pichani Mkuu wa Msafara wa wawekezaji 20 toka Taiwan Eduardo Wang kushoto akimpatia
Kaimu Rais wa chama Cha wafanyabiashara wenye Viwanda, Kilimu (Tccia) Octavian
Mshiu nembo ya “dragon” ambayo ni heshima ya juu yenye kuwakilisha Nguvu, Afya
na Bahati Kadiri ya Mila na Desturi ya sehemu kubwa ya Mashariki ya Asia ikiwa
ni ishara ya Shukrani kwa TCCIA kwa kuratibu vizuri.Picha na mpiga picha wetu.
Wawekezaji wa Tamzania wamepata fursa pekee ya kukutana na wawekezaji
hao huku lengo la wawekezaji hao likiwa na nia ya kushirikiana wawekezaji
wa ndani katika kuelekea uchumi wa viwanda.
Akizungumza Dar es Salaam Kaimu Rais wa Chama Cha TCCIA Octavian Mshiu amesema
kuwa katika ujio huo wawekezaji wa Taiwan ndio waliokuwa wa kwanza kutaka
kufanya maongezi hayo ya kibiashara na wawekezaji wa Tanzania.
"Tumefurahi sana kwa msafara wa wekezaji 20 wenye makampuni mbali mbali
kutua nchini kwa lengo la kutaka kushirikiana na wafanya biashara wenye
viwanda kwani itasaidia mchakato wa Tanzania kufikia uchumi wa wiwanda,"alisema
Octavian.
Octavian alisema kuwa makampuni hayo ya ang'ambo uenda sasa kutaendelea
kupungua kwa tatizo la vifungashio kwani wamiliki hao wanaviwanda vingi
vya vifungashio pamoja utengenezwaji wa malighafi zingine.
Naye Mkuu wa Msafara wa wawekezaji toka Taiwan Eduardo Wang alisema
kuwa wao kama wamekezaji wamefurahishwa na wawekezaji wa Tanzania.
Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambayo ni Taasisi kuu ya Serikali ya kuratibu,
kuhimiza, kukuza na kuwezesha uwekezaji nchini Tanzania na kuishauri kuhusu sera ya uwekezaji na masuala yanayohusiana na uwekezaji hadi sasa kimekuwa kikifanya juhudi kubwa kufikia mafanikio
katika kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.
Ambapo kwa sasa TIC imekuwa ikitaja kuweka na kudumisha mazingira mazuri
ya uwekezaji kwa sekta binafsi.
Comments