UGONJWA wa moyo (presha) ambao ni kati ya
magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa ambapo asilimia ya wagonjwa wa ugonjwa huo
haioneshi kupungua tokea Shirika la Afya Duniani lilipo toa ripoti yake 2012.
Hayo yalibainishwa leo na Mwenyekiti wa Chama cha ugonjwa wa
kisukari Tanzania na Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo yakuambukizwa Profesa Andrew
Swai, wakati wa kampeni ya kupima kwa hiari magonjwa ya kuambukizwa iliyofanyika
katika viunga vya Chuo kikuu huria cha Tanzania jijini Dar es Salaam.
Blog hii lilitaka kufahamu zaidi nini sababu zaidi na nini
kifanyike,Profesa Swai alisema kuwa tatizo kubwa lipo katika ulaji usiofaa
,kwakuwa watu wamekiuka misingi ya ulaji usiofaa na badala yake hujilia kwa
kadri wawezavyo hivyo ameitaka jamii kuzingatia ulaji unaofaa.
Profesa Swai alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la
Afya duniani za mwaka 2012 na tafiti zinazofanywa marakwamara na Chama cha
ugonjwa wa kisukari, inaonesha plesha ni ugonjwa unaongoza kuliko magonjwa yote
yasiyo kuwa ya kuambukizwa.
Ripoti ya ya WHO ya 2012 inaonesha wagonjwa wanaougua plesha
wanaongoza kwa aslimia 26, sukari asilimia 9, na hata baada ya utafiti huo
imeonekana ugonjwa wa plesha umeongezeka mara tatu kuanzia 2012.
“Kwa muda mrefu
tulikuwa tukielimisha ulaji unaofaa kila tunapopata fursa yakuzungumza na
watanzania lakini bado jamii haizingatii ulaji bora na salama nakuwakumbusha
umuhimu waulaji unaozingatia kiasi na si bora ulaji,”Alisema
Hata hivyo Profesa Swai amewataka watanzania kufanya mazoezi
kila siku walau dk 30 za kuuweka mwili vizuri ili kukabiliana na magonjwa
yasiyo yakuambukizwa kwakuwa magonjwa hayo ndiyo magonjwa yanayoongoza kwa vifo
vingi barani Afrika.
Naye Meneja Mradi wa chama cha magonjwa yasiyokuwa
yakuambukizwa Happy Nchimbi, alisema kuwa lengo kubwa lakufanya kampeni hiyo
chuoni hapo ni katika kuhakikisha kuwa walimu na wanafunzi wanaosoma uwalimu
wanaelewa umuhimu wakupima magonjwa yasiyo yakuambukizwa ili watakapo kuwa
mashuleni iwe rahisi kuwaelimisha wanafunzi umuhimu wakupima afya zao.
“Kampeni hii ina lengo la kuvifikia vyuo vya uwalimu na na
shule za msingi na sekondari kwakuwa serikali ina mpango wakurekebisha mitaala
ya elimu nchini nakupendekezwa magonjwa yasiyo yakuambukizwa kuingizwa katika
mitaala ya elimu nchini hivyo imetulazimu kuanza kampeni hii,”Alisema
Happy aliwataka wananchi kwa ujumla kujitokeza kupima katika
kampeni hiyo kwakuwa hutolewa bure na hivi karibuni watakuwa chuo cha uwalimu
Butimba Jijini Mwanza na baadae kampeni hiyo itaendeshwa katika mashule baada
ya shule kufunguliwa.
Juma Salum ni miongoni mwa wananchi walijitokeza kupima afya
,alisema kuwa kampeni hiyo ni nzuri na inawafaa watu wa uchumi wa chini kwakuwa
hutolewa bure lakini kikubwa amefahamu ana damu kiasi gani,plesha kiasi gani na
sukari kiasi gani na kusema kuwa atarekebisha mwenendo wake ya maisha ili asije
athirika na moja ya magonjwa yasiyokuwa yakuambukizwa.
“Binafsi zoezi ni zuri kilichonigusa kwanza ni bure halafu ni
vipimo vya uhakika lakini nishafahamu afya yangu cha msingi nikuzingatia yale
nliyoelekezwa na Daktari,”Alisema
Comments