Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) limewataka wanachama wake
kuwa waaminifu na waadilifu ili kulinda heshima ya chombo hicho pamoja
na kuifikisha nchi katika uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI Dkt.
Samuel Nyantahe wakati wa makabidhiano ya ofisi na Mwenyekiti mpya wa
shirikisho hilo,Surbash Patel yaliyofanyika katika ofisi za CTI jijini
humo.
“Tunakaribisha wenye viwanda kujiunga na na CTI kutokana na ukweli kwamba
tuna viwanda vingi lakini wanachama ni wachache, pia tunasisitiza nidhamu,
uadilifu na uaminifu kwa wanachama,”anasema.
Nyatahe amesema shirikisho hilo lina jumla ya viwanda 1600 lakini kuna
wanachama zaidi 400 huku akiwawataka wenye viwanda ambao hawajiunga kujiunga
na shirikisho ili kulifanya liwe imara zaidi.
Dkt. Nyantahe amemkumbusha mwenyekiti mpya kuendelea kushughulikia
changamoto zinazolikabili shirikisho hilo ikiwemo Sera ya mambo ya kodi
ambayo hubadilika badilika, ucheleweshaji wa kurejeshewa Kodi ya Ongezeko
ya Mapato (VAT), kuchelewa kutoa vibali vya kazi, kupandisha kwa ushuru wa
forodha kwa bidhaa zinazotoka nje pamoja na uwepo wa nishati ya umeme ya
uhakika.
“Sauti ya viwanda itakuwa kubwa tutakapokuwa na wanachama wengi kwakuwa umoja
ni nguvu utengano ni udhaifu,”alisema
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya Surbash Patel amemshukuru mwenyekiti aliyemaliza
muda wake na kuahidi kufuata nyayo zake na kuendelea kumtumia mtangulizi wake katika
masuala yanayohitaji ufafanuzi zaidi.
“Nitashirikiana na wafanyakazi wenzangu pamoja na wanachama,kupaza sauti katika
kushughulikia changamoto zinazohusu viwanda nchini,”anasema.
Surbash amebainisha kuwa atahakikisha CTI inafanya kazi kwa karibu zaidi
na Serikali ya Awamu ya Tano ili kufanikisha adhima uchumi wa kati kupitia
sekta hiyo ifikapo mwaka 2020.
Ameongeza kuwa katika uongozi wake atawasaidia wanachama kutatua changamoto
zao lakini hatakuwa tayari kuwasaidia wanachama watakao kwenda kinyume na
sheria zinazoongoza CTI.
Naye Makamu Mwenyekiti wapili wa CTI, Shabbiri Zavery alitoa wito kwa watanzania
kuthamini,kupenda na kununua bidhaa za ndani ili kujenga uchumi wa Tanzania.
“Ninawahimiza watanzania waone fahari ya kutumia bidhaa zinazo zalishwa nchini
kwakufanya hivyo viwanda vyetu vitakua na mtaji wakuzalisha bidhaa bora,”anasema.

Comments