TIGANYA VINCENT
RS TABORA
JUMLA ya wanawake 46,158 mkoani Tabora wamejifungua katika kipindi cha kuanzia Januari hadi kufikia Septemba mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu wa Afya wa Mkoa wa Tabora Tausi Yunge wakati wa mkutano wa wadau wa faya wa Mkoa huo.
Alisema walijifungua chini ya umri wa miaka 20 walikuwa 11,332 ambao ni sawa na asilimia 24.5 na wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini waliojifungua walikuwa 34,826 sawa na asilimia 75.4.
Tausi alisema watoto waliozaliwa wakiwa hai walikuwa 45,336 sawa na asilimia 98.7 na wasio hai walikuwa 563 sawa na asilimia 1.2.
Kaimu Katibu Afya Mkoa huyo alisema jumla ya wanawake waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma walikuwa ni 43,991 sawa na asilimia 95.3.
Wakati huo huo Kaimu Katibu huyo wa Afya Mkoa amesema kuwa hadi hivi sasa ni Wazee 32,470 sawa na asilima 50 ya wazee 71,116 ya waliotambuliwa ndio wameshapewa vitambulisho kwa ajili ya matibabu mkoani humo.
Alisema ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ndio inaoongoza kwa kutoa kwa wazee 6,700 kati ya 9,766, kufuatiwa na Kaliua iliyotoa kwa wazee 3,700 kati ya 6,019, Uyui 4,000 kati ya 6,840 na Urambo imetoa kwa wazee 5,120 kati ya 9,387.
Tausi alisema Halmashauri ambazo bado ziko chini ni Manispaa ya Tabora ambayo imetoa vitambulisho kwa wazee 600 kati 9,475, Sikonge imetoa kwa wazee 600 kati ya 3,580, Mji Nzega imetoa kwa wazee 1,803 kati ya 5,421 na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imetoa kwa 9,947 kati 20,628.
Kufuatia zoezi hilo kwenda polepole Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa wiki moja kwa wahusika wote kuhakikisha wamekamilisha kazi ya utoaji wa vitambulisho kwa wazee wote wanaonzia miaka sitini na kuendelea.
Alisema baada ya muda huo kupitia ataanza kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika nafasi zao wanaohusika.
Comments